PR. MIGOMBO.
•••••••√••••••••√••••••••√•••••••√••••••••√••••••√•••••
√ Siri
za Unyumba Wenye Furaha.
•Mithali 3:5-7
6 Katika njia zako zote mkiri yeye,Naye atayanyosha mapito
yako.
7 Usiwe mwenye hekima machoni pako;Mche BWANA, ukajiepushe
na uovu.
- Kuwa na Ndoa Yenye Furaha Si Bahati Ya Mtu. Hakuna bahati
katika Ndoa, maana mambo yote yanayofanyika ni matokeo ya kazi ya pamoja
yaletayo furaha baina ya wanandoa.
- Kubali kukifunza pamoja na wengine, wekeza sehemu tofauti
tofauti. Tumia muda mwingi katika mambo yenye faida.
- Jifunze kuangalia kwenye ndoa nyingine zilizofanikiwa.
Kukoseana ni kawaida katika Ndoa jifunze namna nzuri ya kuomba msamaha
unapokosea na kusamehe unapokosewa.
- Aina ya Ndoa utakayokuwa nayo, inategemea wewe ni Mtu wa
Namna Gani. Jitathmini mapungufu yako kama ni MKOROFI, UNA HASIRA, WIVU, KATIRI
au tatizo jingine na uyashughulikie kabla ya kuingia katika maisha na mwenzi
wako. Lishughulikie jambo hilo mapema maana linaweza kuathri ndoa yako...
Nukuu...
"Aina ya ndoa utakayokuwa nayo, inategemea ww ni mtu wa aina
gani....Ikiwa wewe ni mtu wa Furaha ndoa yako inaweza kuwa na Furaha siku
zote"
Dondoo...
"Ili kuwa na furaha lazima ukumbuke mambo yafuatayo,,,
1 -FURAHA
KATIKA NDOA SIO KITU PEKEE CHA MUHIMU KATIKA NDOA. Kama furaha imepungua fanya
mamb yatakayorejesha furaha.
2 - MUME NA MKE UNATAMBUA THAMANI YA KUWEPO, KUDUMU NA
KUJIHUDHURISHA. Mambo yakiwa Magumu usibabaike kupita kiasi, tulia tu na ujue
namna nzuri ya kuishi na Mwenzi wako.
3 -
USIFANYE MAMBO KWA MAZOEA. Acha kufanya mambo kwa mazoea, usiache kumuonyesha
kuwa unampenda acha mazoea katika maisha na mwenzi wako. Fanya kila kitu kipya
ukijua ya kwamba kuna mtu anaekuona na kujihudhurisha. Usiwe wa Kawaida sana
kila siku JALI HISIA ZA MWENZI WAKO na UMUONE KUWA WA THAMANI KILA SIKU.
4 -
MTAZAMO RAFIKI NI WA MUHIMU SANA. Badili mtazamo wako uwe chanya kila siku,
acha kusema sema maneno yanayoonyesha mtazamo HASI mbele ya mwenzi wako. Mfn
"Wanawake bwana siku hizi wana matatizo" Mbele ya mwenzi wako
hukuondolea imani kwake maana umemshusha thamani. Maneno unayoyazungumza
tafadhari yasije kuathiri maisha yako, usimtukane na kumfokea mbele ya watu na
watoto wako.
5 -
BADILISHA FIRKA POTOFU, KABLA YA KUBADILISHA NDOA YAKO.
6 -
Unaweza kubadilisha ndoa yako kwa kufanya mabadiriko yako binafsi. Hakuna mtu
aliye na uwezo wa kumbadirisha mwenzi wake. Lakini ni msukumo wa ndani Ya Mtu
Mwenyewe unaofanya mavadililo ndani yake.
7 - Katika
ndoa Yenye mafanikio mume nanmke huishi kwenye maisha ya Sasa Sio Maisha ya
Jana na Juzi. Acha kuishi maisha yaliyojaa kinyongo. Acha kukumbusha mambi ya
nyuma kila siku.
8- Kuwa
na matatizo hainamaanishi kwamba ni mwisho wa Ndoa. Vumilianeni dhoruba katika
ndoa ni kawaida. Songa mbele kuna njia ya
kutokea.
9- MAJANI
YANAKUWA YA KIJANI UNAPOMWAGILIA. Ndoa ni shule ambayo ukiingia unapewa cheti
cha Kuingia katika Ndoa na hakuna cheti cha kuhitimu. Lakini Lazima ufanye
bidii katika kuhakikisha unafauru katika shule hiyo. Jishughulishe katika ndoa
yako ili uing'arishe Ndoa Yako.
- Ndoa
inafananishwa na Bustani ambayo kila siku inahitajinkutunzwa na kumwagiliwa kwa
usahihi kila siku. Ndoa Pia lazima imwagiliwe kila siku na ingarishwe siku
zote.
- Ndoa pia
inafananishwa na kazi. Cheti hukusaidia kupata kazi lakini hakikusaidii kudumu
katika kazi hivyo ili ubaki katikankazi lazima ujibidiishe na uwajibike na
mwajiri wako akuone bora na wa manufaa kwake. Ndoa pia inahitaji kujibidiisha
na kuwajibika ili ionekani ya thamani siku zote. Fanya hali yako katika maisha
ionekane inaboreka na ya kupendeza kila siku.
FURAHA KATIKA NDOA HAILETWI NA MTU MWINGINE BALI NI WEWE
MWENYEWE NA MWENZI WAKO. ITAFUTE FURAHA KWA KUJITATHIMINI UNALETA MCHANGO UPI
ILI KUIDUMISHA FURAHA YAKO.
Ahsante Na Mungu Akubariki Unapokwenda Kuwa Na FURAHA katika
Ndoa Yako.
Imeandaliwa na:
Sabuya_Jr96
+255 766 060 303 Calls
+255 718 002 992 Whatsapp
Facebook: Sabuya Jr Willy
Instagram: sabuya_jr
Twitter: @willysabuya
barakamarwerwe@gmail.com
No comments:
Post a Comment