Zipo Njia Nyingi za Kuleta Furaha Katika Ndoa
1) Kumsikiliza Mungu2) Kuzikilizana Sisi kwa sisi
3) Kudumisha Upendo
4) Kujifunza kutoa na kupokeaMsamaha
5) Kuwafundisha watoto namna nzuri ya maisha
Mambo yanayoweza kudumisha Upendo Katika Ndoa.
Waefeso 5:33.Jifunze kuishi kwa upendo. Mambo baadhi ni haya hapa;
1) Kuwa na mtazamo Chanya.
- Jitahidi kuwa na mtazamo chanya kwa Mwenzi wako, hata kama itatokea hali ngumu ya maisha, uchumi, kugombana na mengine mengi KUWA NA MTAZAMO chanya.
- Usiwe mtu wa kufikiria Mabaya mabaya tu kila siku. Hata kama jambo gumu limetokea, USIWE TOO SERIOUS, UTAKUFA HARAKA...hahahahahaaaa
- Hata watoto wanapokuwa ndani ya Nyumba bila kuona Baba na Mama wanapendana wanaweza kuathirika na kuwa namatatizo kiasi fulani. Jenga familia Yenye Furaha kuanzia kwa wazazi mpaka Kwa Watoto. Waambie watoto mambo ya upendo na uwajengee kujiamini. "Waambie kuwa unawapenda, waambie kuwa watafanikiwa"
- Ni kawaida katika ndoa na mahusiano hali inaweza kuwa mbaya na kusababisha hasira ikapanda. KAMWE USIZUNGUMZE
- Hasira inapopanda tafuta mahali pa kupumzika, usije ukazungumza kwa hasira ukajuta baadae. Nenda hata bustanini, nenda ukalime, nenda ukatembee itakusaidia kupunguza hasira. Ukiwa nanhasira usiongee na mwenzi wako.
- Mume na mke mjifunze kuwa watoaji sio wapokeaji tu. Lazima kila mmoja awe mtoaji.