Wednesday, June 11, 2014

Shirika la Oxfam, limeanzisha shindano la kombe la dunia mbadala.


Shirika la kutoa huduma za kibinadamu Oxfam limeendesha 'kombe la dunia mbadala' kuangazia pengo linalozidi kuwa kubwa kati ya maskini na matajiri katika mataifa yanayoshiriki kombe la dunia mwaka huu.
Ubelgiji imetangazwa mshindi kwa sababu si kuwa ina utajiri si haba bali pia ina mwanya mdogo zaidi kati ya raia wake matajiri na wenye kipato, ilhali wenyeji Brazil imefeli hata kufuzu raundi ya pili kwa jinsi pengo la umaskini na matajiri lilivyokumbwa miongoni mwa raia wake.
Mataifa mengineyo ya America kusini pia hayajafanya vizuri lakini yanasemekana kujitahidi, cha ajabu mataifa ya kiafrika yanayoshirki kombe la dunia hayajatajwa.

Ulaya wataka Blatter ajiuzulu


Maafisa wa kandanda wa Europa sasa wamemtaka rais wa shirikisho la kimataifa la kandanda FIFA, Sepp Blatter, ajuzulu kutokana na madai ya rushwa yanayoindama Fifa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka Uingereza , Greg Dyke,amesthtumu kauli ya Blatter kuwa madai ya rushwa kuhusiana na kuchaguliwa kwa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2022 yanayoripotiwa katika magazeti ya Uingereza yamechochewa na ubaguzi wa rangi.Mkuu wa chama cha soka cha uholanzi Michael Van Praag, amesema chini ya uongozi wa Blatter ,Fifa imeandamwa na tuhuma za rushwa na ili Fifa kujisafisha ni sharti Blatter angatuke.
Blatter anatarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania nafasi kipindi cha tano kuingoza Fifa katika uchaguzi wa Fifa unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Kwa sasa wajumbe wa Fifa wanavikao huko Sao Paulo wakijiandaa kwa ufunguzi wa kombe la dunia hapo kesho ambako Sepp Blatter pia amekuwa akitoa cheche za maneno dhidi ya wale wanaoisema vibaya Fifa na Qatar.

Vita vya kikabila vyatokota Somalia


Somalia inakumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe
Takriban watu 7 wameuawa nchini Somalia katika vita vya kikabila mkoa wa Galgaduud, katikati mwa Somalia.
Hii inakuja wakati kuna vita vingine vya kikabila kule Marka, kilomita 90, kusini mwa mji mkuu Mogadishu.

Kabila mbali mbali zimeanza kuzozania utawala wa maeneo hayo.Miezi miwili baada ya wanajeshi wa muungano wa Afrika kudhibiti takriban miji kumi katikati na kusini mwa Somalia, vita vya kikabila vimemeanza kuzuka katika baadhi ya maeneo yanayosimamiwa na serikali ya Somalia.
Serikali ya Somalia, imeagiza pande zinazopigana kusitisha vita na kumaliza tafauti kati yao kwa kuzungumza.
Mkuu wa mkoa wa Galgaduud, ameiambia Idhaa ya Kisomali ya BBC kuwa, wanajaribu kusuluhisha tofauti kati ya jamii tafauti, ingawa hawana uwezo wa kijeshi. Amesema wanajeshi wao wanasimamia miji na siyo vijijini ambako vita vimezuka.

Waasi 100 wauawa Kordofan,Sudan

Waasi wa SPLMN wanasema ni wapiganaji watatu tu waliouawa

Jeshi nchini Sudan linasema kuwa limewaua zaidi ya waasi 100 katika jimbo la Kordofan Kusini.
Msemaji wa jeshi Sawarmi Khaled Saad anasema kuwa mauaji hayo yalifanyika wakati wa mapigano yaliyodumu muda wa saa tatu ya kuzima shambulizi eneo la El Atmor.

Kundi hilo limekuwa likiipiga vita serikali ya Khartoum eneo hilo kwa kipindi cha miaka 20 sasaWaasi kutoka kwa kundi la (Sudanes Peoples Liberation Movement North) walithibitisha shambulizi hilo na kusema kuwa ni wapiganaji watatu tu waliouawa.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na vita nchini humo.
Vita hivyo vimezuka wakati Rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wa Sudan Kusini wakitarajiwa kukutana leo kwa mazunguzmo ya amani , ukiwa mkutano wa kwanza katika kipindi cha mwezi mmoja na wa pili tangu vita kuzuka nchini Sudan Kusini.