Wednesday, October 31, 2012

P -SQUARE

P -SQUARE WAKANUSHA KUMTOA KAFARA MAMA YAO





Mapacha wa kundi la P-Square la nchini Nigeria hatimaye wamefunguka kuzikanusha tetesi kuwa walimtoa kafara mama yao mzazi ili watajirike na kufanikiwa zaidi kimuziki.


Katika mahojiano exclusive na gazeti la Vanguard la nchini Nigeria, Peter na Paul wamesema,

“Basi, ni mbaya sana kusikia kuwa watu wanatushutumu kwa kuhusika na kifo cha mama yetu. Hatumlamu mtu yeyote. Watu wako huru kusema chochote wanachotaka kusema. Tunashangaa kama kuna kitu chochote kitakachotufanya tuchukue maisha ya mama yetu mpendwa.

Maisha yake hayawezi kupimwa kwa fedha na umaarufu. Hivyo jibu letu kwa swali hili ni kwamba hatuhusiki na kifo cha mama yetu. Tunakilaumu tu kifo kilichomchukua mbali nasi ambacho kama si chenyewe watu wasingekuwa wanatunyooshea vidole. Alifariki baada ya ugonjwa wa muda mfupi.”

No comments: