Tuesday, December 18, 2012

Azam waitandika Simba

  Michezo » 

, Yanga waua 'Uhai Cup'

17th December 2012
Chapa
Timu ya mpira wa miguu ,Azam Fc.
Mabingwa watetezi wa michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Kombe la Uhai), Simba walijikuta wakiangukia pua jana baada ya kupata kipigo cha mabao 3-2 katika mechi yao kali ya mashindano hayo dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.

Adam Adam aliifungia Azam magoli mawili na Joseph Kimwaga akafunga jingine kuihakikishia Azam ushindi, huku magoli ya Simba yakiwekwa wavuni na Miraji Madenge na Mohamed Salum.

Katika mechi nyingine iliyochezwa jana asubuhi, yosso wa Yanga waliibuka kidedea baada ya kuishindilia Kagera Sugar mabao 6-2.

Mashindano hayo ya kila mwaka huandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuzishirikisha timu za vijana za klabu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Simba walitwaa ubingwa wa michuano hiyo msimu uliopita.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments: