Ngassa: Nina ofa nono zaidi
18th December 2012
Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa, amesema kwamba
anataka suala la yeye kukataa kujiunga na klabu ya El Merreikh ya Sudan
lisiwe gumzo kwani anaamini maamuzi hayo aliyafanya kwa usahihi baada
ya kupata 'ofa' nyingine nono zaidi kuliko kujiunga na timu hiyo ya
Omdurman jijini Khartoum.
Ngassa aliliambia NIPASHE jana kwamba maamuzi yake si ya kukurupuka na amewashirikisha wazazi na familia yake.
Mshambuliaji huyo alisema kwamba ameahidiwa kupewa dau zaidi ya dola za Marekani 50,000 (Sh. milioni 78) ambazo angepata kutoka El Mereikh, nyumba, usafiri atakaouchagua na mishahara ya miezi sita ambayo atalipwa kwa pamoja.
Nyota huyo aliyetua Simba kwa mkopo akitokea Azam alisema kwamba anaamini katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara yeye atakuwa ni mchezaji anayelipwa vizuri kati ya wachezaji wachache wa ligi hiyo inayoendeshwa na kusimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
"Hivi sasa siwezi kuweka kila kitu wazi kwa sababu ni maisha yangu, pia itaniwekea picha mbaya na wachezaji wenzangu," alisema Ngassa ambaye hivi karibuni alikuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Yanga.
Alisema kwamba atahakikisha anaitumikia vyema Simba katika kipindi kilichobakia cha mzunguko wa pili huku akiiweka zaidi timu ya taifa (Taifa Stars).
"Kuna mambo yanaendelea kuhusu mimi, ni wazi kwamba kama mwajiri wako asipokutendea haki ni vigumu kufanya kazi vizuri, ila kwa sasa naomba nisiweke wazi jambo lolote mpaka mechi yetu za Zambia ipite, najua maisha wanayoishi wachezaji wa zamani, sitaki nami inikute hali hiyo," alieleza Ngassa.
Alisema pia bado klabu ya Maritzburg ya Afrika Kusini anawasiliana nao na wameahidi kuzungumza naye mwakani na hawatakuwa na tatizo la kuvunja mkataba ambao atakuwa ameingia na klabu nyingine ya hapa nchini.
Alieleza kwamba hapo awali wachezaji walikuwa wanakurupuka katika kuingia mikataba na hatimaye kujikuta wanawafaidisha viongozi sasa mambo yamebadilika.
Alisema kwamba si kila anayekwenda kucheza nje atapata mafanikio, bali hata hapa nchini ukijipanga hakuna kitakachoharibika.
"Sijutii na wala siwezi kusikitika, nimefanya maamuzi yatakayonilinda mimi na si kuwafurahisha watu," alimaliza nyota huyo.
Baada ya mpango wa kumbakisha nchini Ngassa, kufanikiwa wachezaji wengine wanaotakiwa Yanga ni pamoja na beki, Shomary Kapombe na Emmanuel Okwi, wote wanaichezea Simba na wanamikataba.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment