Friday, February 22, 2013

HUYU NDIO SHABIKI WA MIAKA 14 ALIEFARIKI KWENYE MECHI DHIDI YA CORITHIANS.

Posted: 22nd February 2013 
.
Shabiki mmoja wa kiume wa club ya San Jose mwenye umri wa miaka 14 amefariki kutokana na firework kwenye mechi ya Copa Libertadores ambapo San ilicheza na Corithians.
Kevin Douglas Beltran Espada ni mwanafunzi wa high school kutoka Bolivia ambapo alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali akiwa ameumia machoni pia.
Hilo tukio lilitokea muda mfupi tu baada ya Corithians kupata goli kwenye hiyo mechi iliyochezwa Jesus Bermudez stadium ambapo mashabiki ndio walianza kufyatua firework.
.
Kwa mujibu wa Fox News, Doctor José Maria Vargas aliviambia vyombo vya habari kwamba shabiki huyo alijeruhiwa kwenye fuvu la kichwa na kwenye akili ndio maana kifo chake kilitokea kirahisi.
Polisi wamesema tayari mashabiki tisa wa Brazil wanashikiliwa pamoja hati zao za kusafiria ambapo inaelezwa mashabiki wengine wa Brazil walilazimika kukaa kwa muda uwanjani baada ya mechi kumalizika wakihofia kupigwa na mashabiki wenyeji.
.
Mmoja wa watuhumiwa.

No comments: