Msanii wa bongomovie na bongoflava Hemed Suleiman amepata ajali ambayo imemsababishia kupata maumivu sehemu za kifua baada ya kujigonga akiwa
ndani ya hilo gari. Jerry wa Ryhmes mshikaji wa karibu wa Hemed alielezea
kuhusu ajali hiyo
“Hemed amepata ajali maeneo ya Kijitonyama, baada ya
ajali hiyo amepata maumivu maeneo ya kifuani. Amefikishwa
hospitali kwa ajili ya uchunguzi na amepewa tiba pamoja na
dawa za kutumia. Hivi sasa amepumzika kwake naamini
anaendelea vizuri. Hajapata ajali kubwa sana na kitu kizuri ni
kwamba mashabiki wake na marafiki kupitia mitandao ya
kijamii wamekuwa wakimpa pole na kumtakia apone haraka ”
– Jerry
No comments:
Post a Comment