Zipo Njia Nyingi za Kuleta Furaha Katika Ndoa
1) Kumsikiliza Mungu2) Kuzikilizana Sisi kwa sisi
3) Kudumisha Upendo
4) Kujifunza kutoa na kupokeaMsamaha
5) Kuwafundisha watoto namna nzuri ya maisha
Mambo yanayoweza kudumisha Upendo Katika Ndoa.
Waefeso 5:33.Jifunze kuishi kwa upendo. Mambo baadhi ni haya hapa;
1) Kuwa na mtazamo Chanya.
- Jitahidi kuwa na mtazamo chanya kwa Mwenzi wako, hata kama itatokea hali ngumu ya maisha, uchumi, kugombana na mengine mengi KUWA NA MTAZAMO chanya.
- Usiwe mtu wa kufikiria Mabaya mabaya tu kila siku. Hata kama jambo gumu limetokea, USIWE TOO SERIOUS, UTAKUFA HARAKA...hahahahahaaaa
- Hata watoto wanapokuwa ndani ya Nyumba bila kuona Baba na Mama wanapendana wanaweza kuathirika na kuwa namatatizo kiasi fulani. Jenga familia Yenye Furaha kuanzia kwa wazazi mpaka Kwa Watoto. Waambie watoto mambo ya upendo na uwajengee kujiamini. "Waambie kuwa unawapenda, waambie kuwa watafanikiwa"
- Ni kawaida katika ndoa na mahusiano hali inaweza kuwa mbaya na kusababisha hasira ikapanda. KAMWE USIZUNGUMZE
- Hasira inapopanda tafuta mahali pa kupumzika, usije ukazungumza kwa hasira ukajuta baadae. Nenda hata bustanini, nenda ukalime, nenda ukatembee itakusaidia kupunguza hasira. Ukiwa nanhasira usiongee na mwenzi wako.
- Mume na mke mjifunze kuwa watoaji sio wapokeaji tu. Lazima kila mmoja awe mtoaji.
- Unaweza kuwa Wa Muda wako.
- Ifanye kila saa ambayo anakuwa na wewe aikumbuke kuwa na wewe.
- Waweza Kumtia Moyo Pia. Sio lazima umpe makubwa.
- Msaidie hata kufanya kazi ndogo ndogo
- Vitu unavyotoa lazima viendane na matendo unayoyafanya.
- Wakati wote kila mtu ana udhaufu wake, kama unataka kudumisha upendo katika hali hii fanya hili;
- Tafuta angalau vitu vitatu ambavyo unajua mwenzi wako anavifanya vizuri. Hivi vitasaidia kukumbusha mazuri yake wakatiwa tabu na marumbano.
- Mwambie vitu hivi hata kama vikiwa vingi, mwambie kila kitu kizuri unachokifikiria kwake.
- Mtazame mtu katika ubora wake.
- Kila mtu ana maisha yake, kama ukitaka kulinganisha kila siku UTAKUFA HARAKA. Jua kujifunza vitu vizuri kutoka kwawengine sio kujigunza.
- Udhaifu wa kujilinganisha ni huu;
- Utaiondoa ile furaha iliyopo hata kidogo, yaweza kutoweka na kukufanya uishi maisha ya utumwa.
- Jifunze usiwe na wivu.
- Mambo haya yakifanywa kwa uaminifu mkubwa yaweza kusaidia kuongeza furaha katika ndoa.
Imeandaliwa na;
Sabuya_Jr96
The University Of Dodoma
Dodoma: Tz
No comments:
Post a Comment