Monday, December 17, 2012

Sunday, December 16, 2012

HII NI NYUMBA YA BIBI WA BAGAMOYO ALIYE VAMIWA NA MAJAMBAZI WIKI ILIYO PITA.



Jina lake ni Mwajuma Masaigana mwenye umri wa miaka 61 ambae december 8 ameingia kwenye headlines za AMPLIFAYA ya CLOUDS FM baada ya kutangazwa na polisi kwamba amefanikiwa kuua jambazi kwa risasi, jambazi moja kati ya nane waliomvamia nyumbani kwake wakiwa na bunduki, hapo juu kwenye kioo ni moja ya madirisha ya sebuleni kwake ambayo yalitumika kurushiana risasi na hao majambazi.
Matobo ya risasi.
.
.
Wakati majambazi wanarushiana risasi na bibi walikua huku chini.
Hili jiwe walitumia kuvunjia mlango wa chini ambako ndio kulikua na mali nyingi sana lakini hawakuchukua hata moja, walisema tu wanataka kujua bibi alipo wamuue.
Hiyo mbao mpya inayoonekana imewekwa baada ya mlango kuvunjwa.
Ngazi za kupanda chumbani kwa bibi ziko kwa nje kwa hiyo majambazi walipogundua bibi anaishi juu wakapanda mpaka kwenye mlango wa kuingilia.
.
.
Hapa ndio mlango wa kuingilia kwa bibi, walipokuta grill wakaanza kuvunja ili wauvunje na mlango wa mbao kisha wamfate bibi aliyekua na bunduki pia, mpaka wanapanda hapa juu ilikua tayari kama dakika 20 zimepita toka warushiane risasi na bibi bila mafanikio, wakati wakiwa hapa mlangoni bibi akiwa ndani alipata akili ya kupiga risasi kupitia mlango wa mbao ambayo ilitoka nje na kumpiga jambazi mmoja aliefariki palepale.
Hapa ndio kwa ndani bibi akionyesha madirisha mawili aliyotumia kurushiana nao risasi, hilo kochi hapo kushoto ndio alikua anajibanza baada ya kupiga risasi.
.
.

.
.
.
Huu ni mlango wa mbao ambao risasi ndio ilipita na kumuua huyo jambazi.
.
Mama Masaigana akionyesha sehemu aliposimama wakati anapiga hiyo risasi.
Hapa ndio jambazi aliangukia baada ya kupigwa risasi na wenzake 7 waliobaki wakakimbia.
Huyu ndio Mama Masaigana ambae aliwahi kuwa mwanajeshi kwa kipindi cha mwaka mmoja miaka ya 80, may 2013 anafikisha umri wa miaka 62… mpaka sasa yeye ni mmiliki wa shule mbili za primary zilizosajiliwa Serikalini, anasema amekua akipokea vitisho vingi kwenye simu yake kutokana na kazi yake na pia kutokana na ishu ya mtoto wake wa kiume kutaja majambazi ambayo yaliwahi kumvamia nyumbani kwake.
.
Hapa ni Bagamoyo Pwani Tanzania, hii nyumba kaijenga karibu kabisa na bahari ya hindi yani akifungua tu mlango wa uwani anaingia baharini.
.
.
.
 Picha na millard ayo.

MATOKEO YA JANA YA Barclays Prem