Sunday, October 28, 2012

SOCCER

2MAN VS CHELSEA



Wachezaji wa Manchester wakisherehekea bao
Wachezaji wa Manchester wakisherehekea bao..


Timu ya Manchester United imeifunga Chelsea katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge kwa jumla ya magoli 3 - 2 katika mechi iliyochezwa siku ya Jumapili.

Katika mechi hiyo wachezaji wawili wa Chelsea Fenarndo Torres na Branislav Ivanovic walitolewa baada ya kupewa kadi nyekundu na kuwapa nafasi Manchester United kutumia upungufu huo kutawala mchezo.

Katika mechi nyingine iliyochezwa siku ya Jumapili Newcastle imeifunga West Bromwich Albion kwa magoli 2 - 1 , huku Liverpool ikishindwa kulinda magoli yake mawili iliyoyapata kipindi cha kwanza pale ilipocheza na Everton na kutoka sare ya magoli 2 -2.

Mechi nyingine iliyochezwa hapo Jumapili ilikuwa kati ya Tottenham na Southampton ambapo Tottenham ilitoka kifua mbele baada ya kukandamiza Southampton magoli 2 - 1 magoli yaliyofungwa na Gareth Bale na Clint Dempsey.

MAN U BEATS CHELSEA

THESE ARE PICTURES OF MANCHER VS CHELSEA,







soccer

BURKINA FC YATANDIKWA NA MKAMBA RANGERS 1-0 JAMHURI MOROGORO.- LIGI DARAJA LA KWANZA


Mshambuliaji wa timu ya soka ya Mkamba Rangers Msafiri Makambi kulia akichuana na mchezaji wa Burkina FC, Saidi Manga wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza uliowakutanisha timu zote za mkoa wa Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa ambapo katika mchezo huo Burkina ilifungwa bao 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Mkamba Rangers Msafiri Makambi kulia akichuana na mchezaji wa Burkina FC, Saidi Manga wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza uliowakutanisha timu zote za mkoa wa Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa ambapo katika mchezo huo Burkina ilifungwa bao 1-0.

TIMU ya soka ya Burkina FC imeendeleza kugawa pointi mbele ya Mkamba Rangers katika mchezo zote za Morogoro katika mkali wa ligi daraja la kwanza baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kikiwa ni cha pili mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.

Mshambuliaji Athman Msafiri ndiye aliyezamisha jahazi la Burkina FC baada ya kuifungia timu yake bao katika dakika ya 76 kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliochingwa na Kamugisha Edson nje ya 18 kufuatia mlizni wa Burkina FC, Peter Damian kumfanyia madhambi mchezaji wa Mkamba Rangers na kufunga bao hilo lililomuacha Mohamed Barakati asijue la kufanya na mpira kujaa wavuvi.

Licha ya kupata kipigo hicho cha kupoteza mchezo wa pili pia kocha mkuu wa timu hiyo ya Burkina FC, Damian Mussa amejikuta akimaliza mchezo katika jukwaa la mashabiki baada ya kuondolewa katika benchi la ufundi na mwamuzi wa mchezo huo Mary Kapinga kutoka Songea dakika ya 44 kufuatia kutupiana maneno makali na mashabiki wake.

Katika mchezo huo Burkina FC walicheza chini ya uwezo wao na kusababisha kukaribisha mashambulizi ya mara kwa mara lango kwao baada ya kushindwa kucheza kwa maelewano huku Mkamba wakitumia nafasi hiyo kutengeneza mashambulizi kwa wapinzani wao.

Kocha mkuu wa Mkambara Rangers Keneth Mkapa alisema kuwa ushindi huo umempa faraja na kuongezea morali kwa wachezaji baada ya kupoteza mchezo wao wa ufunguzi na kufungwa bao 2-0 na Polisi Iringa wakati mchezo ujao ukitarajia kucheza na Small Kids ya Rukwa Oktoba 31 mkoani Rukwa huku Kocha wa Burkina akishindwa kupatiakana kuzungumzia mchezo huo.

Wakati Mkamba ikitarajia kucheza na Small Kids katika mchezo wa tatu yenyewe Burkina FC itachuana na Majimaji ya Songea Oktoba 31 kwenye uwanja wa Majimaji mwaka huu baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza na Mbeya City kwa kupachikwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Jamhuri.