Timu
ya Manchester United imeifunga Chelsea katika uwanja wake wa nyumbani wa
Stamford Bridge kwa jumla ya magoli 3 - 2 katika mechi iliyochezwa siku ya
Jumapili.
Katika mechi hiyo
wachezaji wawili wa Chelsea Fenarndo Torres na Branislav Ivanovic walitolewa
baada ya kupewa kadi nyekundu na kuwapa nafasi Manchester United kutumia
upungufu huo kutawala mchezo.
Katika mechi nyingine
iliyochezwa siku ya Jumapili Newcastle imeifunga West Bromwich Albion kwa magoli
2 - 1 , huku Liverpool ikishindwa kulinda magoli yake mawili iliyoyapata kipindi
cha kwanza pale ilipocheza na Everton na kutoka sare ya magoli 2
-2.
Mechi nyingine
iliyochezwa hapo Jumapili ilikuwa kati ya Tottenham na Southampton ambapo
Tottenham ilitoka kifua mbele baada ya kukandamiza Southampton magoli 2 - 1
magoli yaliyofungwa na Gareth Bale na Clint Dempsey.