ORODHA YA NYOTA 23 WANAOWANIA TUZO YA FIFA Ballon d'Or.... AFRIKA NZIMA WAMO DIDIER DROGBA NA YAYA TOURE TU... REAL MADRID YATOA NYOTA SITA, BARCELONA YATOA WACHEZAJI WATANO, MANCHESTER CITY WATATU....!
ZURICH,
Usiwsi
STRAIKA wa timu ya taifa ya Argentina na
klabu ya Barcelona, Lionel Messi yuko mbioni kuandika rekodi ya kuwa mtu wa
kwanza kushinda tuzo ya Mwansoka Bora wa Mwaka wa Dunia kwa mara ya nne
mfululizo baada ya kujumuishwa katika orodha iliyotolewa leo na Shirikisho la
Soka la Kimataifa (FIFA) kuwania tuzo hiyo ya
Straika huyo mwenye miaka 25, aliyeongeza
idadi ya mgoli yake tangu aanze kucheza akiwa na klabu na timu ya taifa hadi
kufikia 301 Jumamosi, ni miongoni mwa nyota 23 waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo,
wengine wakiwa ni hasimu wake, straika wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa
ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ambaye alishika nafasi ya pili katika tuzo
zilizotolewa mwaka jana na Messi kuibuka kidedea.
Andres Iniesta wa Barcelona, aliyetajwa kuwa
mchezaji bora wa fainali za Euro 2012 baada ya kuisaidia Hispania kutwaa ubingwa
pia amejumuishwa katika orodha hiyo kama ilivyo kwa Radamel Falcao, ambaye
amekuwa akionyesha kiwango cha juu cha upachikaji mabao akiwa na timu yake ya
taifa ya Colombia na klabu ya Atletico Madrid, akiisaidia nchi yake kutwaa
ubingwa wa Ligi ya Europa msimu uliopita.
Kocha wa Barca, Tito Vilanova amemwagia sifa
Messi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo.
"Sidhani kama tutapata nafasi ya kuona tena
mchezaji kama yeye. Sio tu kwa sababu ya mabao anayofunga lakini pia kwa uwezo
wake wa kusoma mchezo," alisema kabla ya kumsiofia pia Iniesta.
"Yeye (Iniesta) ni mfano kwa wachezaji
wanaolelewa Masia (shule ya soka ya vijana wa Barcelona) na kufikia kiwango cha
juu. Ni mchezaji mwingine miongoni mwa wenye viwango vya juu na ambao Barca
itapata wakati mgumu wa kuwaibua tena."
Makocha 10 pia wametajwa kuwania Tuzo ya
Kocha Bora wa Mwaka wa Dunia, akiwamo Vicente del Bosque, aliyeiongoza Hispania
kutwaa ubingwa wa fainali za Euro 2012 zilizofanyika Julai nchini Ukraine na
Poland.
Roberto Di Matteo, aliyetwaa nafasi ya
kuiongoza Chelsea miezi miwili kabla ya kutwaa taji la Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya mwezi Mei, pia amejumuishwa katika orodha hiyo ambayo hata hivyo
haikumjumuisha Mfaransa Herve Renard aliyeiongoza Zambia kutwaa ubingwa bila
kutarajiwa katika fainali za Kombe Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi
Februari.
Orodha hiyo fupi itachujwa zaidi na kubaki
watu watatu kufikia mwishoni mwa Novemba huku mshindi akitarajiwa kutangazwa
duniani kote kupitia matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya sherehe za
kukabidhi tuzo zitakazofanyika mjini Zurich, Uswisi Januari 7 mwakani.
Wachezaji (kwa kuzingatia mpangilio wa herufi
za majina yao):
1. Sergio Aguero (Argentina)
2. Xabi Alonso (Hispania)
3. Mario Balotelli (Italia)
4. Karim Benzema (Ufaransa)
5. Gianluigi Buffon (Italia)
6. Sergio Busquets (Hispania)
7. Iker Casillas (Hispania)
8. Cristiano Ronaldo (Ureno)
9. Didier Drogba (Ivory Coast)
10. Radamel Falcao (Colombia)
11. Zlatan Ibrahimovic (Sweden)
12. Andres Iniesta (Hispania)
13. Lionel Messi (Argentina)
14. Manuel Neuer (Ujerumani)
15. Neymar (Brazil)
16. Mesut Ozil (Ujerumani)
17. Gerard Pique (Hispania)
18. Andrea Pirlo (Italia)
19. Sergio Ramos (Hispania)
20. Wayne Rooney (England)
21. Yaya Toure (Ivory Coast)
22. Robin van Persie (Uholanzi)
23. Xavi (Hispania).
Makocha (kwa kuzingatia herufi za kwanza za
majina yao pili):
1. Vicente del Bosque (Hispania/taifa
Hispania)
2. Roberto Di Matteo
(Italia/Chelsea)
3. Alex Ferguson (Scotland/Manchester
United)
4. Pep Guardiola (Hispania/kocha wa zamani
Barcelona)
5. Jupp Heynckes (Ujerumani/Bayern
Munich)
6. Jurgen Klopp (Ujerumani/Borussia
Dortmund)
7. Joachim Low (Ujerumani/taifa
Ujerumani)
8. Roberto Mancini (Italia/Manchester
City)
9. Jose Mourinho (Ureno/Real
Madrid)
10. Cesare Prandelli (Italia/taifa
Italia)
No comments:
Post a Comment