MENEJA
wa klabu ya Polisi Moro Sport Club na Msemaji wa klabu hiyo, Clement Bazo
amesema kuwa klabu yake itaibuka na ushindi dhidi ya vinara wa ligi kuu ya
vodacom Tanzania bara klabu ya Simba katika mchezo wao wa ligi hiyo utaopigwa
kesho kwenye uwanja wa Jamhuri majira ya saa 10:30 mkoani hapa.
Bazo
alisema kuwa mchezo huo utakuwa mchezo wao wa tisa tangu kuanza kwa ligi hiyo na
kupoteza michezo sana na kutoa sare mbili na kujikusanyia pointi mbili
wanauchukua mchezo huo kama michezo mingine baada ya kufanya vibaya hivyo lengo
kuu ni kufanya vizuri na kuwa wamejindaa kukabiliana na vinara
hao.
“Tumefanya
maandalizi ya kutosha kwa michezo iliyobakia hivyo kesho (leo) tunacheza na
Simba hivyo sisi Polisi lengo letu tulilonalo kwa sasa ni kufanya vizuri ukiwemo
mchezo wetu dhidi ya dhidi ya Simba SC na tunaasilimia 75 ya ushindi kwa mchezo
huo”. Alisema Bazo.
Bazo
alisema kuwa mchezo ni mchezo matokeo ambayo yanahitajika katika mchezo huo kama
watashindwa kuwafunga Simba basi mchezo utaweza kumalizika kwa sare ya aina yo
yote ile.
Naye
Kocha Mkuu wa klabu ya Polisi Sport Club, John Simkoko amesema maandalizi ya
mchezo wao dhidi ya Simba yamekabili na anachosubiri ni dakika 90 kuweza kuamua
matokeo ya mchezo huo.
Akizungumza
na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es Salaam ambako wameweka
kambi katika jeshi la polisi Kulasini, Simkoko alisema kuwa wachezaji wake wote
wapo fiti kwa mchezo huo na anachosubiri ni kuanza kwa mchezo huo dhidi ya
vinara wa ligi ligi Simba Sport Club hii kesho.
Simkoko
alisema kuwa waliweka kambi mapema katika jiji hilo baada ya mchezo wao dhidi ya
Ruvu JKT kwa lengo kumalizia michezo iliyobakia ukiwemo na Simba katika uwanja
wake wa nyumbani na kuwa dakika 90 ndizo zitakazoamua mshindi katika mchezo wa
soka.
“Mchezo
utakuwa mgumu kwa pande zote mbili na tumejiandaa vya kutosha kwa ajili ya
kuikabili Simba hivyo najua Simba wanahitaji ushindi nasi vile vile tunahitaji
ushindi katika mchezo huo lakini dakika 90 ndizo siku zote zinaamua matokeo ya
mchezo ikiwemo sare, kupoteza na ”. alisema Simkoko.
Katika
mchezo huo utanarajia kuibua hisia nyingine kutoka kwa mashabiki Manispaa ya
Morogoro endapo klabu hiyo ya Polisi Moro kama itaendelea kupoteza mchezo huo
baada ya kupoteza mwelekeo kufuatia kufungwa michezo saba na sare mbili huku
ikiwa na pointi mbili
No comments:
Post a Comment