WAZIRI Mkuu Mstaafu , Edward Lowassa, amesema unyonge wa elimu
kwa watoto wa kike hautamalizwa kwa kelele za wanasiasa , bali ni kwa taifa
kuweka misingi imara itayowasaidia kujielimisha kadili ya ukomo wao, ili wawe
na uwezo wa kutosha wa kupambana na changamoto zinazowakabili.
Kauli hiyo aliitoa jana Jijini hapa, wakati akiendesha harambe
ya kuchangia ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha
Teofilo Kisanji (TEKU),kinachomilikiwa na kanisa la MoravianiTanzania (KMT) na
kufanyika katika usharika wa Ruanda jimbo la kusini Magharibi.
Katika harambe hiyo Lowassa alichangia fedha taslimu kiasi cha
shilingi milioni 25, huku viongozi mbalimbali wa serikali na chama tawala (CCM)
wakiongozwa na na Mkuu wea Mkoa wa Mbeya,Abas Kandoro aliyewakilishwa na Mkuu
wa wilaya ya Rungwe Chrispine Meela nao wakitoa mchango wao.
Lowasa alisema ili taifa liweze kujidhatiti kikamilifu ni lazima
watu wake wakaona fursa na kuamua kuwekeza kwenye elimu , ambapo kundi kubwa la
vijana wataweza kujifunza na kuelimika katika mambo mbalimbali.
Alisema jitihada za kuwakomboa wanawake hususani watoto wa kike
haziishi tu kwa viongozi wa siasa kupiga kelele majukwaani, bali ni watanzania
kuwajengea uwezo wa kila hali ili kuhakikisha wanasoma kwa kadili ya ukomo wao.
Akizungumzia vijana kwa ujumla Lowassa alisema wanapaswa
kutambua kuwa elimu ndio njia pekee ya wao kujikatika changamoto mbalimbali,
hivyo bila nyenzo hiyo hawawezi kufika mahala popote, badala yake fursa
mbalimbali zitawapita na wao kubaki watazamaji.
“Baba Askofu kwani hata ukitaka kufuga kisasa au kibiashara
lazima uwe na elimu, na hata wale waliojiandaa kufanya kazi za ofisini wanakuwa
na hali ngumu bila kuwa na elimu ya kutosha” alifafanua Lowassa.
Aliwata vijana kutumia vizuri fursa walizopata za kusoma katika
vyuo vikuu iwe kwa ufadhili wa watu au serikali kwani watu hao waliowafadhili
walijinyima kwa malengo ya kuhakikisha wanawatimizia matakwa yao ambayo ni
faida kwa taifa pia.
Hata hivyo alisema kama vijana wa Tanzania hawataelimika vya
kutosha katika elimu ya juu hawataweza kutoa ushindani wa kutosha kwa wenzao
kwenye soko la ajira kwa nchi za zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alinikuu kifungu cha Biblia “ Tumeambiwa katika bibilia
takatifu…tusipojibiidisha kutafuta maarifa tutaishia kuwa wateka maji, wakata
kuni kwa wenzenu (Joshua 9:21), kwa hiyo nalipongeza kanisa la Moraviani kwa
bidii na umoja wao kwa kujenga chuo kikuu.”
Aidha, Lowassa aliweka wazi kuwa tabia yake ya kuchangia katika
makanisa ni wito na kamwe yeye si tajiri bali amekuwa ana changiwa na baadhi ya
marafiki zake wanaoshirikiana hivyo kupata fedha hizo ambazo anazitoa kwenye
harambe m,balimbali anazoombwa kuendesha na kuchangia.
“Mimi naenda sana kwenye harambe sijafirisika, lakini mimi sio
tajiri kama watu wanavyosema ila huwa nachangiwa na wenzangu na hivyo kuwa na
nguvu ya kuchangia kwenye makanisa kama mtakavyoona leo” alisema Lowassa.
Hata hivyo Lowassa alilipongeza kanisa hilo kwa utulivu kwa
kusema ni tofauti na miaka iliyopita kwa kanisa hilo kuandamwa na migogoro
mingi ambayo ilisababisha kanisa kukosa utulivu na kuwayumbisha waumini wake.
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa kanisa hilo Jimbo la Kusini
Magharibi, Alinikisa Cheyo, katika harambee hiyo lilitarajia kukusanya kiasi
cha shilingi milioni 500 ili kuweza kumalizia ujenzi wa mabweni kwea wanafunzi
wa kike katika chuo hicho.
|
No comments:
Post a Comment