Meneja Mahusiano wa
Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza na wanafunzi wa shule
mbalimbali za Sekondari za jijini Dar kuhusiana na shindano kubwa
lililoshirikisha wanafunzi kutoka nchi zote za Afrika la kuandika Insha na
kuchora picha kuhusiana na mambo ya Anga linaloitwa DStv EUTELSAT STAR AWARDS
ambapo mshindi wake atapata nafasi ya kwenda Paris nchini Ufaransa na wazazi
wake kushuhudia namna safari ya kwenda mwezini inavyofanyika kabla ya
kumkaribisha Mwanaanga wa Kwanza Afrika Kwenda mwezini Patrick Baudry ambaye
atazungumza nao kuhusiana na uzoefu wake kuhusiana na masuala ya
Anga.
Barbara amesema kwamba
mshindi wa shindano hilolililodhaminiwa na Dstv atatangazwa hapo kesho katika
hafla maalum ya chakula cha jioni itakayofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency
Kilimanjaro.
Mwanaanga wa kwanza kutoka
Barani Afrika kwenda mwezini Patrick Baudry leo ametoa mafunzo kwa wanafunzi
shule za Sekondari za jijini Dar es Salaam juu ya mpangilio mzima wa safari ya
kwenda mwezini na kurudi tena duniani.
Baudry ametoa mafunzo hayo
katika ukumbi wa Nkurumah ikiwa ni semina maalum kwa wanafunzi wa shule za
sekondari hapa nchini ambao wameshiriki kwenye shindano kubwa la kuandika Insha
na kuchora picha kuhusiana na masuala ya Anga. Baudry mwenye umri wa miaka 66 ni
mzaliwa wa Cameroon.
Baadhi ya Wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Hindu Mandal.
Baadhi ya wanafunzi wa
Shule ya Sekondari Jangwani wakitega sikio kwa umakini.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mwanaanga Patrick Baudry
(hayupo pichani) aliyezungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Ukumbi
wa Nkuruma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.
Patrick Baudry akijibu
maswali aliyokuwa akiulizwa na wanafunzi hao. Kulia ni Barbara
Kambogi.
Mwanafunzi wa Shule ya
Sekondari Jangwani akiuliza Swali kwa Mwanaanga Patrick Baudry (hayupo pichani)
wakati akizungumza na Wanafunzi jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Walimu wa shule
mbalimbali nchini waliombatana na wanafunzi wao.
Patrick Baudry akitia
saini Autograph za Wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha maswali na
majibu.
No comments:
Post a Comment