Thursday, November 29, 2012

YATIMA WA TANZANIA WAPATA SHIRIKA LITAKALO WASAIDIA.

Shirika lisilo la kiserikali la Jamhuri ya Czech BEZ MAMY limeanza kampeni ya kukusanya pesa Ulaya kwa ajili ya Kusaidia watoto yatima nchini Tanzania hasa mkoani Mbeya

Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia akiwa na wadau wa Czech BEZ MAMY 
Michoro ya picha za tingatinga inayotumika kukusanya michango hiyo
Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia akiendesha moja ya semina za kuchangia mfuko huo

Shirika lisilo la kiserikali la Jamhuri ya Czech BEZ MAMY limeanza kampeni ya kukusanya pesa Ulaya kwa ajili ya Kusaidia watoto yatima nchini Tanzania hasa mkoani Mbeya
Bez Mamy kwa kushirikiana na shirika la Kitanzania la jiji Mbeya Without Mother Organization kwa pamoja wamedhamiria kuinua elimu mkoani Mbeya kwa kusaidia ukarabati na utoaji wa misaada kwa shule za msingi jijini Mbeya, Ujenzi wa vituo vya watoto yatima, kuwalipia ada watoto yatima na kuboresha huduma za Afya jijini na wilaya mbalimbali za mkoa wa Mbeya
Akiongea na blog hii Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia alisema, wanatumia njia mbalimbali kukusanya pesa  hizo ambazo zitatumika katika ujenzi wa Bweni la wasichana katika kituo cha watoto yatima Mahango,Mswiswi pamoja na ujenzi wa Sekondari ya Ufundi katika Kijiji hicho cha Mahango
Njia zinazotumika kukusanya pesa hizo ni uuzaji wa michoro ya Tinga Tinga katika sehemu Mbalimbali nchini Slovakia na Jamhuri ya Czech na pia kupitia mtandao www.tingatingashop.cz
Njia nyingine ni utoaji wa Mihadhari katika vyuo vikuu, shule za sekondari za ufundi, Makanisani na kwa watu binafsi katika nchi hizo
Akizungumzia misaada na miradi hii bwa Chris Zacharia alisema,Ikiwa watu wa Ulaya wanajitoa kusaidia watoto wa afrika itawatia moyo zaidi kusaidia ikiwa watasikia watanzania wengine wenye uwezo pamoja na serikali wanajitoa kusaidia kundeleza miradi hii ambayo ina msaada mkubwa kwa uchumi na maeneleo ya nchi yetu

No comments: