14th December 2012
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana, kocha huyo raia wa Denmark alisema kuwa ameamua kuingiza ‘sura’ mpya katika kikosi chake kutokana uwezo uliooneshwa na wachezaji hao katika mashindano mbalimbali yakiwamo ya ligi kuu.
Katika kikosi hicho, wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Aishi Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam FC na timu ya taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na mshambuliaji wa Azam FC, Mcha Khamis.
Pia kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichoshika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kampala, Uganda.
Wachezaji hao ni Mwadini Ally, Nassoro Masoud ‘Chollo’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis.
Kikosi kamili kilichoitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam U20). Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Masoud ‘Cholo’ (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih Nuhu (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).
Viungo ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga), Mrisho Ngasa (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe).
Washambuliaji ni John Bocco ‘Adebayor’ (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe) na Mwinyi Kazimoto (Simba).
KATONGO, KALABA, SUNZU WAJA
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema jana kuwa tayari Chama cha Soka cha Zambia (FAZ) kimeshaweka wazi orodha ya wachezaji wa Chipolopolo watakaotua jijini Dar es Salaam Desemba 18 kwa ajili ya kuikabili Stars.
Alisema kuwa kikosi cha wachezaji 24 kilichotajwa na kocha Chopolopolo, Herve Renard, kinaundwa na Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
No comments:
Post a Comment