Waombolezaji
Katika mazishi hayo, Rais Jakaya Kikwete aliwakilishwa na kaka
yake Selemen Kikwete ambaye pia alipata nafasi ya kutoa pole kwa waombolezaji
ambao hawakuruhusiwa kuuona mwili wa marehemu bali kilichoruhusiwa kuangaliwa
ni picha yake iliyokuwa juu ya jeneza.
Mbali na Seleman Kikwete, viongozi mbalimbali nwalihudhuria
msiba huo akiwemo Mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa Taifa Tanzania Ndugu
Othuman, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya mstaafu John Mwakipesile na viongozi
kadhaa waandamizi wa Serikali.
Marehemu Mwasokwa akatwa na kitu chenye ncha kali kisogoni
ambako wauaji ambao hawajajulikana walifanya kitendo hicho kisha kuulaza mwili
wake kifudifudi nje ya geti la nyumba yake eneo la Block T jijini Mbeya.
Taarifa za Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, zimesema kuwa wauaji
wanaonekana kuwa walitumia panga ambapo marehemu alikutwa na majereha makubwa
sehemu za shingoni, kichwani, mabegani na mkono wa kushoto.
No comments:
Post a Comment