CHADEMA WAVUNJA MASANDUKU NA KUIBA FEDHA ZA UCHAGUZI.
Vurugu Chunya
WATU 13 akiwemo diwani wa viti maalumu kupitia Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kata ya saza Benadetha Zacharia(38)
wanashikiliwa na jershi la polisi kwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu
wa mali ya umma yakiwemo masanduku ya kupigia kura.
Wengine ni katibu wa Chadema kata ya Saza wilayani Chunya
Braison Mwasimba(34),John Mponzayo(52),Seleman Tanganyika(24),Ambokile
Francis(23),Amos Joseph(24),Abdul Mwandeule(20),Christopher Mwanjayo(37),
Baraka Saul(19),Musa Mnyonga(32),Essa Pius(18),Marco Gibson(25) wote wakazi wa
kata ya Saza na Paradiso Emanuel(26) mkazi wa kijiji cha Njenjele wilayani
Mbeya. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman alisema kuwa mnamo desemba 8
mwaka huu majira ya saa 11:15 katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Saza
baadhi ya wananchi wakiongozwa na watuhumiwa waliamua kujichukulia sheria
mikononi na kusababisha uharibifu wa mali za umma. Kamanda Athuman alitaja
uharibifu uliofanyika kuwa ni kuvunjwa kwa kioo cha mbele cha gari yenye namba
SM 3830 Toyota Landcruiser mali ya halmashauri ya wilaya ya Chunya,kuvunja
mlango na dirisha la ofisi ya afisa mtendaji kata. Alisema hbaada ya uharibifu
huyo watuhumiwa waliingia ndani ya ofisi hiyo na kuharibu masanduku 24 ya
kupigia kura ambapo thamani ya mali zote bado haujafahamika. Alisema chanzo cha
vurugu hizo ilikuwa kushinikiza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kujaza
nafasi ya mwenyekiti wa kijiji na vitongoji uliokuwa ufanyike siku ya jumapili.
Kufuatia vurugu hizo uchaguzi huo ililazimu kusogezwa mbele siku moja na
kufanyika jana(Disemba 10) huktaratibu za kisheria zikiendelea ikiwemo
kufikishwa jana mahakamani katioka mahakama ya wilaya ya Chumnuya watuhumiwa 12
na kusomewa mashitaka. Ukiachilia mbali shitaka la uharibifu wa mali za umma
linalowakabili washitakiwa wote mahakamani hapo washitakiwa Amos Joseph,Braison
Mwasimba na Paradiso Emanuel wanakabiliwa na shitaka jingine la unyang’anyi.
Alisema washitakiwa hao walifanya unyang’anyi wa fedha kiasi cha shilingi
2,150,000 zilizokuwa sehemu ya gharama za uchaguzi,simu ya kiganjani na saa ya
mkononi
|
No comments:
Post a Comment