Wednesday, June 11, 2014

Vita vya kikabila vyatokota Somalia


Somalia inakumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe
Takriban watu 7 wameuawa nchini Somalia katika vita vya kikabila mkoa wa Galgaduud, katikati mwa Somalia.
Hii inakuja wakati kuna vita vingine vya kikabila kule Marka, kilomita 90, kusini mwa mji mkuu Mogadishu.

Kabila mbali mbali zimeanza kuzozania utawala wa maeneo hayo.Miezi miwili baada ya wanajeshi wa muungano wa Afrika kudhibiti takriban miji kumi katikati na kusini mwa Somalia, vita vya kikabila vimemeanza kuzuka katika baadhi ya maeneo yanayosimamiwa na serikali ya Somalia.
Serikali ya Somalia, imeagiza pande zinazopigana kusitisha vita na kumaliza tafauti kati yao kwa kuzungumza.
Mkuu wa mkoa wa Galgaduud, ameiambia Idhaa ya Kisomali ya BBC kuwa, wanajaribu kusuluhisha tofauti kati ya jamii tafauti, ingawa hawana uwezo wa kijeshi. Amesema wanajeshi wao wanasimamia miji na siyo vijijini ambako vita vimezuka.

No comments: