Jeshi nchini Sudan linasema kuwa limewaua zaidi ya waasi 100 katika jimbo la Kordofan Kusini.
Msemaji wa jeshi Sawarmi Khaled Saad anasema kuwa mauaji hayo yalifanyika wakati wa mapigano yaliyodumu muda wa saa tatu ya kuzima shambulizi eneo la El Atmor.
Kundi hilo limekuwa likiipiga vita serikali ya Khartoum eneo hilo kwa kipindi cha miaka 20 sasaWaasi kutoka kwa kundi la (Sudanes Peoples Liberation Movement North) walithibitisha shambulizi hilo na kusema kuwa ni wapiganaji watatu tu waliouawa.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na vita nchini humo.
Vita hivyo vimezuka wakati Rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wa Sudan Kusini wakitarajiwa kukutana leo kwa mazunguzmo ya amani , ukiwa mkutano wa kwanza katika kipindi cha mwezi mmoja na wa pili tangu vita kuzuka nchini Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment