Wednesday, March 14, 2018

SOMO: MAHABA KATIKA NDOA.


PR. CALEB MIGOMBO
Nini Maana Ya Neno Hili?
Mwanzo 2:18,22-

  • Mpango wa Mungu Kwa Mwanadamu, aliumba vitu vyote na kuona viko sawa na viliwekwa kila kiumbe viwili viwili. Lakini Adamu Aliumwa Peke Yake. Mungu alimweka Adam katika hali ya Kuona hajakamilika na anahitaji  kuwa na mtu anaefanana nae. Na ndio maana akamuumbia Mwanamke, kutoka katika Ubavu katika mbavu zake.
  • Muumbaji alitengeneza mazingira yaliyomwezesha Adamu Kuona ile haja ya Kuwa na Mwanamke..... Leo kila mtu anatafuta mtu wa kufanana nae kwa kuweka sifa fulani kwabsababu ndani Yetu Mungu ametuumbia ile hali ya kutaka kuishi na kufanana nasisi.. Hivyo jitambue wewe ni wa namna gani ndiyo uanze kutafuta mtu wa kufanana naye. JITAMBUE KWANZA.
  • Mwanamume na mwanamke, ataacha Baba na Mama ataambatana na Mume au Mke wake; na HUU NDIO MWANZO WA MAHABA, unaacha kila kitu na kwa ajili ya mwenzako.
AJALI KUBWA....!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  • Ni rahisi sana kwa wanandoa ambao walipendana Sana katika kipindi cha uchumba.
  • Adui mkubwa katika mazingura yetu kwa kipindi hiki katika ndoa zetu ni KAZI NYINGI. Mambo haya yakiendelea kwa muda mrefu hupooza hali ya ndoa na kufanya ionekane ya kawaida. Mambo kama haya hufanya jambo dogo linapotokea kuvuruga familia kushindwa kulitatua maana HAKUNA MAHUSIANO.
NAMNA YA KURUDISHA MAHABA KATIKA NDOA......
1) Anza kumchumbia mke wako Upya.
  •  Kumbuka ulikotoka, kumbuka kipindi mnaanza mahusiano, simulia haya mambo hata kwa watoto wako.
2) Usijisahau.
  • Jitengeneze uvutie na Upendeze. Wanaume vitu vyao vingi viko machoni, Changamoto za ndoa zinaweza kukufanya ukabadilika sana na mwenzi wako akakuona wa kawaida sana. Jaribu kujiweka katika ambayo mwenzi wako atakuona UNAPENDEZA na KUONEKANA VIZURI... Fahari ya Mume ni kukuona Unapendeza sana.
  • JALI USAFI. Hata kama unafanya kazi ngumu na unapoteza muda mwingi katika kazi jitahidi kujitunza na kuhakikisha uko msafi.
  • Usiende kitandani siku moja. Vaa vizuri mpendwa, Nyoa nywele zako kila mahali kuwa msafi zaidi,
3) Andika Orodha ya Vitu vinavyokuvuti kwa Mume au Kwa Mume wako.

4)Mwambie mwenzi wako hitaji Lako.
  • Mwambie mambo ambayo yanakufurahisha akiyafanya na kuyaongea. Fikisha ujumbe kwa mwenzi wako, ONGEA LUGHA YA MAHABA kwa Mwenzi wako. Lugha inabadilika mahali na mahali.. USIONGEE LUGHA YA KANISANI wakati mkiwa chumbani hahahahahaa... Kila jambo lina mahali pake,,, hakuna mahaba ya kuongea kama uko shambani ukiwa chumbani.
5)Tendo la Ndoa ni takatifu halina shida
6) Panga kuwa na muda wa kuongea.
  • Panga wewe na mke wako muwe na muda wa kuongea na kubadilishana mawazo. Tembea nae na watu wengine wamjue, mfanye kuwa wa kwanza katika ndoa yako.
Mungu akubariki unapopanga Kurudisha Furaha Katika Ndoa Yako.....
Ahsante..
Imeandaliwa na;
Sabuya_Jr96
+255 766 060 303 Calls
+255 718 002 992 whatsap
Facebook: Sabuya Jr Willy
Instagram: sabuya_jr
Twitter: @willysabuya
Email: sabuyawilliam@gmail.com

No comments: