Wednesday, November 28, 2012

MAGAZETI YA JUMATANO

28th November 2012   News

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

HAPA NDIPO ALIPO ZIKWA SHALO MILIONEA

Kaburi alipo zikwa sharo milionea
.Enzi za uhai wake sharo milionea.
 

MTOTO AMUUA MAMA YAKE MZAZI KWA NGUMI

story na baraka.


 Akina mama waombolezaji wakisawazisha kaburi la marehemu Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na mwanae Ndele Julius(25)


 Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika Nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya


 Kaburi baada ya kuzikwa marehemu

Mkazi wa  Swaya jijini Mbeya Ndugu Ndele  Julius amemuua mama yake mzazi kwa kumpiga mateke na ngumi kisha kutoroka pasipo julikana Novemba 25 mwaka huu.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa mama huyo mara baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto wake na kijana  mwingine hali iliyopelekea mama huyo kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi  Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya mtoto wake na kijana  mwenzake kitendo ambacho kilipelekea mama huyo kuingilia ugomvi huo .
Amesema wakati  mama huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto wake alicha kupigana na mwenzake na kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga ngumi na mateke mwilini.
Amesema mama huyo alifariki muda mchache kutokana na kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa majeraha makuibwa yaliyopeleka kupoteza uhai wake.
Awali akizungumzia tukio hilo Mtoto wa Kwanza wa mama huyo Ndugu Razaro Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na tabia ya kugombana na mama yake marakwamara .
Hata hivyo teyari mwili huo umekwisha chukuliwa hospitali na kuzikwa ambapo katika maziko hayo Chama cha Muungano wa kijamii (Mujata) umewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji bangi na pombe za kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi.

Tuesday, November 27, 2012

COMENT

WATEJA 42 WA TIGO LEO KUIBUKA WASHINDI KATIKA DROO YA PILI YA SMARTCARD

 

Meneja Intaneti wa Tigo Titus Kafuma (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tigo kuchagua washindi wengine 42 leo mbele ya Revenue Assurance na Bodi ya Usimamizi wa Michezo ya Bahati Nasibu katika droo ya pili ya mwezi ya Jumuiya ya Tigo SmartCard itakayofanya washindi waliochaguliwa mpaka sasa kufikia 84.

MWANAANGA WA KWANZA AFRIKA KWENDA MWEZINI ATOA SEMINA KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI DAR.


Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza na wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari za jijini Dar kuhusiana na shindano kubwa lililoshirikisha wanafunzi kutoka nchi zote za Afrika la kuandika Insha na kuchora picha kuhusiana na mambo ya Anga linaloitwa DStv EUTELSAT STAR AWARDS ambapo mshindi wake atapata nafasi ya kwenda Paris nchini Ufaransa na wazazi wake kushuhudia namna safari ya kwenda mwezini inavyofanyika kabla ya kumkaribisha Mwanaanga wa Kwanza Afrika Kwenda mwezini Patrick Baudry ambaye atazungumza nao kuhusiana na uzoefu wake kuhusiana na masuala ya Anga.
Barbara amesema kwamba mshindi wa shindano hilolililodhaminiwa na Dstv atatangazwa hapo kesho katika hafla maalum ya chakula cha jioni itakayofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro.
Mwanaanga wa kwanza kutoka Barani Afrika kwenda mwezini Patrick Baudry leo ametoa mafunzo kwa wanafunzi shule za Sekondari za jijini Dar es Salaam juu ya mpangilio mzima wa safari ya kwenda mwezini na kurudi tena duniani.
Baudry ametoa mafunzo hayo katika ukumbi wa Nkurumah ikiwa ni semina maalum kwa wanafunzi wa shule za sekondari hapa nchini ambao wameshiriki kwenye shindano kubwa la kuandika Insha na kuchora picha kuhusiana na masuala ya Anga. Baudry mwenye umri wa miaka 66 ni mzaliwa wa Cameroon.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Hindu Mandal.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakitega sikio kwa umakini.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mwanaanga Patrick Baudry (hayupo pichani) aliyezungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Ukumbi wa Nkuruma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.
Patrick Baudry akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na wanafunzi hao. Kulia ni Barbara Kambogi.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani akiuliza Swali kwa Mwanaanga Patrick Baudry (hayupo pichani) wakati akizungumza na Wanafunzi jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Walimu wa shule mbalimbali nchini waliombatana na wanafunzi wao.
Patrick Baudry akitia saini Autograph za Wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu.

Tatiza Network!!


" Tatizo Ni Network......!"

... Haipatikani, mpaka usimame pahala maalum. Pichani ni Pawaga, Iringa.