Silvio Berluscon haukumiwa kwenda jela.
Milan, Itali - 26/07/2012.
Aliyekuwa waziri mkuu wa Itali
amehukumiwa kwenda jela na kuzuiliwa kushiriki katika maswala ya
kiofisi baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka kodi za malipo.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya kukutwa kuhusika katika biashara kinyume na sheria.
Silvio Berlusconi ambaye alikuwa waziri mkuu wa Itali, amehukumiwa kwa
mara ya kwanza, japo hapo awali alishafunguliwa kesi tofauti zidi yake.
Baada ya hukumu hiyo, Berlusconi alisema "hukumu haina maana na haikufuata haki"
Hata hivyo Silvio Berlusconi amekata rufaa baada ya hukumu hiyo.
Rais wa Marekani apiga kura mapema.
Chicago, Marekani - 26/10/2012. Rais wa Marekani amepiga katika
mji wake Chicago ikiwa ni moja ya kampeni za kutaka wapiga kura
wajitokeze kwa wingi.
Rais Baraka Obama, alipiga kura huku kura za maoni zikiwa zimesimama
katikati baada ya mpinzani wake Mitt Romney kujivuta juu katika kura za
maoni zilizo tolewa hivi karibuni.
Upigwaji wa kura hizo ni moja ya mpangilio ya uchaguzi uliyopo nchini Marekani.
Mara baada ya kumaliza kupiga kura Baraka Obama, aliendelea na ziara ya
kampeni ya kutaka raia wa Marekani kumpigia kura hasa katika miji ya
Ohio Virginia na Florida.