Thursday, July 11, 2013

ALIE TUMBUKIZA MTOTO CHOONI HUKO MBEYA AFUNGWA JELE MIAKA MITANO

ALIYE TUMBUKIZA KICHANGA CHOONI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA. (TUNAOMBA RADHI KWA BAADHI YA PICHA ZITAKAZO ONEKANA)

 Rukia Haruna (31) pichani aliye kutwa na hatia ya kutupa mtoto chooni.
 Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela


****************************
HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA JUNI 14 .2013 ENEO LA MANGA A JIJINI MBEYA


*********************
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
 
Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
 
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
 
Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
 
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.

Friday, March 8, 2013

MBUNGE wa Mbeya vijijini (CCM) Lackson Mwanjali ameingia lawamani kwa kutotekeleza ahadi.


 MBUNGE wa Mbeya vijijini (CCM) Lackson Mwanjali ameingia lawamani baada ya wanachi wa Kitongoji cha Italazya kata ya Ilembo Wilaya ya Mbeya kumtuhumu Mbunge huyo kwa kutoa ahadi hewa ambayo ameshindwa kuitekeleza.

Haya ndiyo majengo waliojenga wananchi sasa yanabomoka kwa ahadi hewa ya mbunge




 MBUNGE wa Mbeya vijijini (CCM) Lackson Mwanjali ameingia lawamani baada ya wanachi wa Kitongoji cha Italazya kata ya Ilembo Wilaya ya Mbeya kumtuhumu Mbunge huyo kwa kutoa ahadi hewa ambayo ameshindwa kuitekeleza.
  
Mbunge huyo aliwaagiza wananchi hao kujenga shule ya msingi katika kitongoji chao kutokana na umbali wa shule nyingine inayosababisha watoto kutembea umbali mrefu kufuata shule.
  
Mbunge huyo aliwaambia wananchi hao kujenga majengo ya vyumba vya madarasa hadi kufikia usawa wa mtambaapanya(renta) ambapo yeye atamalizia kupitia mfuko wa jimbo.
  
Hata hivyo kufuatia ahadi hiyo hali hiyo imekuwa kinyume na matarajio ya wananchi hao ambao wamesema tangu atoe agizo hilo mbunge huyo hajawahi kurudi kijijini hapo wala kutekeleza ahadi hiyo.
  
Wananchi hao walisema kufuatia hali hiyo walilazimika kumfuata mara kadhaa mbunge huyo ofisini kwake ili wamkumbushe kuhusu ahadi yake baada ya wao kukamilisha usawa waliopangiwa na mbunge wao lakini waliishia kuahidiwa tu.
Aidha wananchi hao walisema Mbunge huyo amewavunja nguvu baada ya majengo waliojenga kuanza kubomoka hali iliyosababisha kukatishwa tamaa na utekelezaji wa ahadi hiyo.
  
"Tumejaribu kumfuata mara kadhaa ofisini kwake kuhusu kutekeleza ahadi yake hiyo lakini anaendelea kutuahidi hali inayoonesha kutudanganya tu" alisema Adson Kinga mjumbe wa Serikali ya Kitongoji.
  
Alisema juhudi kubwa iliyofanywa na wananchi katika kujenga majengo hayo ambayo walisema ilikuwa ni ukombozi wa watoto wa kutotembea umbali mrefu lakini juhudi hizo zimeyeyuka baada ya jengo kuanguka kutokana na kutoendelezwa.
  
" Ingekuwa ni kilimo tungekuwa tuko kwenye mavuno makubwa kutokana na nguvu tuliyoitumia kujenga madarasa hayo lakini tunasikitishwa na mbunge kutusahau wakati sisi ndiyo tuliomchagua" alisema Furaha Mwafowela mkazi wa Kitongoji hicho.
  
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hiyo hakupokea simu zake za kiganjani ambazo ziliita mda mrefu bila kupokelewa.
(Chanzo Mbeya Yetu)

Friday, February 22, 2013

HUYU NDIO SHABIKI WA MIAKA 14 ALIEFARIKI KWENYE MECHI DHIDI YA CORITHIANS.

Posted: 22nd February 2013 
.
Shabiki mmoja wa kiume wa club ya San Jose mwenye umri wa miaka 14 amefariki kutokana na firework kwenye mechi ya Copa Libertadores ambapo San ilicheza na Corithians.
Kevin Douglas Beltran Espada ni mwanafunzi wa high school kutoka Bolivia ambapo alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali akiwa ameumia machoni pia.
Hilo tukio lilitokea muda mfupi tu baada ya Corithians kupata goli kwenye hiyo mechi iliyochezwa Jesus Bermudez stadium ambapo mashabiki ndio walianza kufyatua firework.
.
Kwa mujibu wa Fox News, Doctor José Maria Vargas aliviambia vyombo vya habari kwamba shabiki huyo alijeruhiwa kwenye fuvu la kichwa na kwenye akili ndio maana kifo chake kilitokea kirahisi.
Polisi wamesema tayari mashabiki tisa wa Brazil wanashikiliwa pamoja hati zao za kusafiria ambapo inaelezwa mashabiki wengine wa Brazil walilazimika kukaa kwa muda uwanjani baada ya mechi kumalizika wakihofia kupigwa na mashabiki wenyeji.
.
Mmoja wa watuhumiwa.

ZIKUFIKIE KUHUSU MECHI YA KWANZA YA DAVID BECKHAM PSG

 

Posted: 22nd February 2013 
.
Taarifa ikufikie kwamba baada ya watu wengi kuwa na hamu ya kufahamu ni lini David Beckam atacheza mechi yake ya kwanza toka ajiunge na club ya PSG ya Ufaransa, jibu limetoka tayari.
Alielitoa ni kocha Ancelotti kwamba Beckham ataingia uwanjani kwa mara ya kwanza akiwa na PSG kwenye mechi dhidi ya Marseille siku ya jumapili.
Marseille iko nafasi ya tatu pointi 5 nyuma ya PSG ambapo kwenye hiyo mechi club hii itamkosa striker Jordan Ayew ambae ana suspension na pia midfielder Benoit Cheyrou ambae ni majeruhi.

RAIS MWAI KIBAKI AKIFUNGUA BARABARA YENYE JINA LAKE DSM

 

Posted: 22nd February 2013 
Zamani ilikua ni Old Bagamoyo road ila kwa sasa ni Mwai Kibaki road, ina kilomita

HIZI NDIO PICHA ZA NYUMBA 5 NILIZOKUCHAGULIA UZITAZAME LEO MTU WANGU

 

Posted: 22nd February 2013
Hii nyumba ipo California Marekani.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Hii nyumba ya pili inayofata iko Hispania.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Hii nyumba ya tatu ipo Mexico.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Nyumba namba 4.
Wakati kukiwa na uwezekano mkubwa wa mto kama huu kufanywa jalala kwa bongo, huko Australia mjanja mmoja ndio kautendea haki kwa namna hii.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Hii nyumba ya 5 iko Chicago Marekani.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Niambie umependa nyumba namba ngapi mtu wangu 
Chanzo millardayo.com.