PR. CALEB MIGOMBO
Nini Maana Ya Neno Hili?
Mwanzo 2:18,22-
- Mpango wa Mungu Kwa Mwanadamu, aliumba vitu vyote na kuona viko sawa na viliwekwa kila kiumbe viwili viwili. Lakini Adamu Aliumwa Peke Yake. Mungu alimweka Adam katika hali ya Kuona hajakamilika na anahitaji kuwa na mtu anaefanana nae. Na ndio maana akamuumbia Mwanamke, kutoka katika Ubavu katika mbavu zake.
- Muumbaji alitengeneza mazingira yaliyomwezesha Adamu Kuona ile haja ya Kuwa na Mwanamke..... Leo kila mtu anatafuta mtu wa kufanana nae kwa kuweka sifa fulani kwabsababu ndani Yetu Mungu ametuumbia ile hali ya kutaka kuishi na kufanana nasisi.. Hivyo jitambue wewe ni wa namna gani ndiyo uanze kutafuta mtu wa kufanana naye. JITAMBUE KWANZA.
- Mwanamume na mwanamke, ataacha Baba na Mama ataambatana na Mume au Mke wake; na HUU NDIO MWANZO WA MAHABA, unaacha kila kitu na kwa ajili ya mwenzako.
- Ni rahisi sana kwa wanandoa ambao walipendana Sana katika kipindi cha uchumba.
- Adui mkubwa katika mazingura yetu kwa kipindi hiki katika ndoa zetu ni KAZI NYINGI. Mambo haya yakiendelea kwa muda mrefu hupooza hali ya ndoa na kufanya ionekane ya kawaida. Mambo kama haya hufanya jambo dogo linapotokea kuvuruga familia kushindwa kulitatua maana HAKUNA MAHUSIANO.
1) Anza kumchumbia mke wako Upya.
- Kumbuka ulikotoka, kumbuka kipindi mnaanza mahusiano, simulia haya mambo hata kwa watoto wako.