Thursday, December 13, 2012

KAULI YA CHADEMA KUHUSU MAGUFULI KUMPIGIA DEBE ODINGA KENYA.



Mkurugenzi wa  mambo ya  nje   na Ushirikiano  wa Kimataifa EZEKIEL WENJE
Mwenyekiti wa  chama cha demokrasia CHADEMA kimeitaka  Serikali kutolea ufafanuzi suala la WazirI wa ujenzi Dr. John Magufulu kuhudhuria  Sherehe  za kutambulishwa kwa mgombea urais chama cha ODM Kenya Raila Odinga endapo suala hilo lina uhusiano wowote wa Kiserikali.
Mkurugenzi wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Ezekiel Wenje amesema kitendo cha waziri huyo kuhudhuria sherehe za kutambulishwa wa Raila kinatoa picha mbaya ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya iliyopo  Madarakani kutokana  na ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali hizo.
kwenye sentensi nyingine Wenje amesema Magufuli kupanda jukwaani kuanza kumnadi kiongozi wa ODM ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za kimataifa ambapo amedai kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa mataifa ni kosa kubwa Taifa moja kuingilia siasa za Taifa jingine hata kama hayo mataifa yanaushirikiano wowote.

No comments: