Amir-Jamaat Ahmadiyya Tanzania, Tahir Mahmood Chaudhry
Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Mkoa wa Mbeya
itafanya mkutano wenye lengo la kuzungumzia mchango
wa dini katika kuleta amani ya taifa na dunia kwa ujumla.
Mkutano huo utafanyika siku ya Jumanne
tarehe 20/08/2013 katika ukumbi wa mikutano wa
Benjamin Mkapa kuanzia saa kumi Alasiri. Inshallah.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo. Aidha
viongozi na watendaji kadhaa wa serikali katika
ngazi mbalimbali mkoani Mbeya pamoja na viongozi
wa Jumuiya za kidini na asasi sisizo za kiserikali
wamealikwa kwenye mkutano huo, na baadhi
yao watapata nafasi ya kuzungumza katika mada
hiyo muhimu.
Jumuiya ya Waisamu Waahmadiyya inauona mkutano
wa aina hii kuwa ni muhimu hasa katika kipindi hiki
ambacho taifa letu linapita katika wakati mgumu
wa mivutano baina ya wanadini wenyewe kwa
wenyewe na wakati mwingine na serikali.
Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya ambayo ni
Jumuiya ya kimataifa ilianzishwa na Seyyidna
Mirza Ghulam Ahmad a.s. katika kijiji cha Qadiani
India mnamo mwaka 1889 kufuatia wahyi
alioupokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba
amemtuma ili kuwa Masihi na Imam Mahdi wa
zama zetu. Hapa nchini Jumuiya ya Ahmadiyya
ilisajiliwa rasmi mwaka 1934.
Tangu kusajiliwa kwake pamoja na kujihusiaha
na masuala ya kueneza dini ya Kiislam
kwa amani, Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya
imesaidia kukuza Lugha ya Taifa kwa kutoa tafsiri
ya kwanza ya Qu’ran Tukufu kwa Kiswahili mwaka 1953.
Jumuiya pia inajihusisha na utoaji wa hudum aza
kijamii na misaada ya kibinadamu kila inapowezekana
hasa kupitia shirika lake la Kimataifa Humanity First.
Jumuiya imeweza kusaidia katika ukarabati wa
visima vya maji safi vipayavyo 50 kwenye maeneo
mbalimbali nchini katika kipindi cha miaka miwili
iliyopita. Pia misaada ya vifaa vya maabara, kompyuta,
mabegi ya shule, kalamu na madaftari ya kuandikia
yametolewa kwenye shule kadhaa nchini yakilenga
zaidi maeneo ya wanaohitaji. Kwa sasa Jumuiya ya
Waislamu Waahmadiyya duniani inaongozwa na
Khalifa wa Tano wa Masihi aliyeahidi Hadhrat
Mirza Masroor Ahmad a.t.b.a. huku ikiwa na matawi
yake katika nchi 202 duniani.
Wassalaam;
________________
Tahir Mahmood Chaudhry
AMIR – JAMAAT AHMADIYYA TANZANIA
No comments:
Post a Comment