Friday, December 14, 2012

BUSOKELO WAPATA VIONGOZI WAPYA.

HALMASHAURI MPYA YA BUSOKELO WAPATA VIONGOZI WAPYA

IMELDA ISHUZA MKURUGENZI HALMASHAURI YA BUSOKELO

MHE,MECKSON MWAKIPUNGA MWENYEKITI  HALMASHAURI YA BUSOKELO

MHE, SALOME MWAKALINGA MAKAM MWENYEKITI HALMASHAURI YA BUSOKELO

BARAZA LA MADIWANI JIPYA LA BUSOKELO WAKIWA KATIKA KIKAO CHA KWANZA CHA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAO

WATENDAJI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO

MR MASANJA AFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO

GIDION MAPUNDA AFISA KILIMO NA MIFUGO HALMASHAURI YA BUSOKELO
HAWA NI BAADHI YA WATENDAJI  WA HALIMASHAURI YA BUSOKELO AMBAYO KWA KUANZIA KUTAKUAWA NA WATUMISHI 386 AMBAO WATASAIDIA KULETA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA BUSOKELO ILIYOUNDWA KUTOKA KATIKA HALMASHAURI YA RUNGWE NA KUFANYA WILAYA YA RUNGWE KUWA NA HALMASHAURI MBILI, RUNGWE NA BUSOKELO.

VURUGU HUKO CHUNYA.

CHADEMA WAVUNJA MASANDUKU NA KUIBA FEDHA ZA UCHAGUZI.

Vurugu Chunya

WATU 13 akiwemo diwani wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kata ya saza Benadetha Zacharia(38) wanashikiliwa na jershi la polisi kwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu wa mali ya umma yakiwemo masanduku ya kupigia kura.
Wengine ni katibu wa Chadema kata ya Saza wilayani Chunya Braison Mwasimba(34),John Mponzayo(52),Seleman Tanganyika(24),Ambokile Francis(23),Amos Joseph(24),Abdul Mwandeule(20),Christopher Mwanjayo(37), Baraka Saul(19),Musa Mnyonga(32),Essa Pius(18),Marco Gibson(25) wote wakazi wa kata ya Saza na Paradiso Emanuel(26) mkazi wa kijiji cha Njenjele wilayani Mbeya. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman alisema kuwa mnamo desemba 8 mwaka huu majira ya saa 11:15 katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Saza baadhi ya wananchi wakiongozwa na watuhumiwa waliamua kujichukulia sheria mikononi na kusababisha uharibifu wa mali za umma. Kamanda Athuman alitaja uharibifu uliofanyika kuwa ni kuvunjwa kwa kioo cha mbele cha gari yenye namba SM 3830 Toyota Landcruiser mali ya halmashauri ya wilaya ya Chunya,kuvunja mlango na dirisha la ofisi ya afisa mtendaji kata. Alisema hbaada ya uharibifu huyo watuhumiwa waliingia ndani ya ofisi hiyo na kuharibu masanduku 24 ya kupigia kura ambapo thamani ya mali zote bado haujafahamika. Alisema chanzo cha vurugu hizo ilikuwa kushinikiza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa kijiji na vitongoji uliokuwa ufanyike siku ya jumapili. Kufuatia vurugu hizo uchaguzi huo ililazimu kusogezwa mbele siku moja na kufanyika jana(Disemba 10) huktaratibu za kisheria zikiendelea ikiwemo kufikishwa jana mahakamani katioka mahakama ya wilaya ya Chumnuya watuhumiwa 12 na kusomewa mashitaka. Ukiachilia mbali shitaka la uharibifu wa mali za umma linalowakabili washitakiwa wote mahakamani hapo washitakiwa Amos Joseph,Braison Mwasimba na Paradiso Emanuel wanakabiliwa na shitaka jingine la unyang’anyi. Alisema washitakiwa hao walifanya unyang’anyi wa fedha kiasi cha shilingi 2,150,000 zilizokuwa sehemu ya gharama za uchaguzi,simu ya kiganjani na saa ya mkononi

UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA WAANZA KUTUMIKA.

LIVEE UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA WAANZA KUTUMIKA NDEGE ZAIDI YA TATU ZATUA

UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA UMEANZA KUFANYA KAZI LEO NDEGE ZAIDI YA TATU ZATUA UWAJANI HAPA
ABIRIA AKISHUKA TOKA NDANI YA NDEGE ZILIZOTUA UWANJANI HAPO

MWANDISHI WA HABARI KAMANGA WA BLOG YA MATUKIO AKISHUKA TOKA KATIKA NDEGE KUZINDUA UWANJA HUO
BAADHI YA WTUMISHI WA UWANJA HUO WAKISHUSHA MIZIGO TOKA KATIKA NDEGE
BAADHI YA ABILIA  WALIOSHUKA UWANJANI HAPO
MAMA HELLEN RAIA WA UGANDA AKIFURAHIA KUTUA KATIKA KIWANJA HICHO CHA SONGWE MBEYA
MWENSHIMIWA DIWANI WA KATA YA SISIMBA G. KAJIGIRI AKISUBIRI MGENI WAKE TOKA DSM
MOJA YA MAAFISA WA UHAMIAJI UWANJANI HAPO

TUTAZIDI KUWALETEA KINACHOJIRI UWANJANI HAPA SONGWE

JK AMTUMA KAKA YAKE MAZISHI YA OFISA USALAMA ALIYEUAWA MBEYA

  MAZISHI YA OFISA USALAMA

MAZISHI ya aliyekuwa ofisa Usalama wa Taifa (mstaafu) mkoa wa Mbeya RSO Joseph Nelson Mwasokwa, aliyeuwawa usiku wa kuamkia Desemba 9, mwaka huu Jijini Mbeya, yamefanyika katika Kijiji cha Ibungu wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Kaka wa rais Kikwete Selemani Kikwete akinigia wilayani kyela kwenye mazishi ya marahamu mzee mwasokwa
Aliyekuwa mkuu wa mkoa mbeya Mwakipesile akiongea na mzee Mwambulukutu kwenye mazishi ya marehemu Mwasokwa
Waombolezaji 

Katika mazishi hayo, Rais Jakaya Kikwete aliwakilishwa na kaka yake Selemen Kikwete ambaye pia alipata nafasi ya kutoa pole kwa waombolezaji ambao hawakuruhusiwa kuuona mwili wa marehemu bali kilichoruhusiwa kuangaliwa ni picha yake iliyokuwa juu ya jeneza.
Mbali na Seleman Kikwete, viongozi mbalimbali nwalihudhuria msiba huo akiwemo Mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa Taifa Tanzania Ndugu Othuman, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya mstaafu John Mwakipesile na viongozi kadhaa waandamizi wa Serikali.
Marehemu Mwasokwa akatwa na kitu chenye ncha kali kisogoni ambako wauaji ambao hawajajulikana walifanya kitendo hicho kisha kuulaza mwili wake kifudifudi nje ya geti la nyumba yake eneo la Block T jijini Mbeya.
Taarifa za Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, zimesema kuwa wauaji wanaonekana kuwa walitumia panga ambapo marehemu alikutwa na majereha makubwa sehemu za shingoni, kichwani, mabegani na mkono wa kushoto.