PR. MIGOMBO.
•••••••√••••••••√••••••••√•••••••√••••••••√••••••√•••••
√ Siri
za Unyumba Wenye Furaha.
•Mithali 3:5-7
6 Katika njia zako zote mkiri yeye,Naye atayanyosha mapito
yako.
7 Usiwe mwenye hekima machoni pako;Mche BWANA, ukajiepushe
na uovu.
- Kuwa na Ndoa Yenye Furaha Si Bahati Ya Mtu. Hakuna bahati
katika Ndoa, maana mambo yote yanayofanyika ni matokeo ya kazi ya pamoja
yaletayo furaha baina ya wanandoa.
- Kubali kukifunza pamoja na wengine, wekeza sehemu tofauti
tofauti. Tumia muda mwingi katika mambo yenye faida.
- Jifunze kuangalia kwenye ndoa nyingine zilizofanikiwa.
Kukoseana ni kawaida katika Ndoa jifunze namna nzuri ya kuomba msamaha
unapokosea na kusamehe unapokosewa.
- Aina ya Ndoa utakayokuwa nayo, inategemea wewe ni Mtu wa
Namna Gani. Jitathmini mapungufu yako kama ni MKOROFI, UNA HASIRA, WIVU, KATIRI
au tatizo jingine na uyashughulikie kabla ya kuingia katika maisha na mwenzi
wako. Lishughulikie jambo hilo mapema maana linaweza kuathri ndoa yako...