Thursday, November 22, 2012
PAKISTANI SHIITE PROCESSION HIT BY BOMBING, 6 DEAD.
ISHTIAQ MAHSUD, Associated Press
Updated 7:53 a.m., Sunday, November 25, 2012
Pakistani Shiite Muslim girls mourn during a Muharram procession in Islamabad, Pakistan, Saturday, Nov. 24, 2012. Muharram is a month of mourning in remembrance of the mn artyrdom of Imam Hussein, the grandson Pakistani Shiite Muslim girls mour
during a Muharram procession in Islamabad, Pakistan, Saturday, Nov. 24, 2012. Muharram is a month of mourning in remembrance of the martyrdom of Imam Hussein, the grandson of Prophet Mohammed. Photo: Anjum Naveed / AP
Pakistani security officials check the site of a bomb blast as the minority Muslim Shia sect observes the annual Ashoura holiday in Dera Ismail Khan, Pakistan, Sunday, Nov. 25, 2012. A bombing claimed by the Taliban killed several people at a Shiite religious procession in northwestern Pakistan on Sunday, police said.
Wednesday, November 21, 2012
POLICE
Polisi Waanda Mpango Mkakati Wa Ulinzi Shirikishi
Mkuu wa Polisi wilaya
ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto akiongea na wakazi wa Mtaa
Kitalu "D" Njiro katika mkutano uliofanyika tarehe 18.11.2012 juu ya uanzishwaji
wa vikundi vya ulinzi shirikishi
Mwenyekiti wa Mtaa wa
Kitalu "D" Njiro Bw.John Kihwele akihesabu fedha zilizopatikana baada ya Mkuu wa
Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto (kushoto
kwake) kuchangisha fedha hizo kwa njia ya harambee katika mkutano
uliowajumuisha, askari Polisi, viongozi wa Mtaa na wakazi wa eneo hilo
uliofanyika tarehe 18.11.2012.Jumla ya fedha taslimu Tsh 125,000 zilipatikana
papo hapo.
Picha na Mahmoud AhmadArusha
Na: Rashid Nchimbi wa
Polisi Arusha
Wakazi
wa Njiro mtaa wa Kitalu “D” wametakiwa kutolifanyia mzaha suala la uanzishaji
wa vikundi vya ulinzi shirikishi kwa madai kuwa wanajitosheleza katika suala
hilo. Akiongea na wakazi hao Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi Gilles Muroto alisema kwamba suala la ulinzi halihitaji ubinafsi wala
masihara bali linahitaji ushirikiano wa hali juu.
“Tatizo
nililoligundua hapa kila mmoja anaona ameshajitosheleza katika suala la ulinzi
kwa kuwa ana mlinzi, kamera na uzio wa umeme, wakati suala hilo linahitaji
ushirikiano mkubwa”. Alionya Muroto .
Aliwataka wakazi hao
wachukue hatua za haraka juu ya uanzishaji wa vikundi hivyo ili kutotoa mwanya
kwa wahalifu kwani udhaifu walionao unaweza kutoa mwanya kwa wahalifu kuvamia
eneo hilo.
Alimuagiza Mwenyekiti wa
mtaa huo kukaa na wakazi hao ili kupitisha maazimio juu ya uchangiaji wa vikundi
hivyo na mara baada ya kukubaliana sheria hiyo itakuwa ni miongoni mwa sheria za
serikali ya mitaa hivyo basi yeyote atakayekaidi atachukuliwa
hatua.
Aidha
aliwataka viongozi wa mtaa huo kuwafahamu watu wote wa eneo hilo hivyo kusaidia
kubaini tabia ya kila mmoja na pia kila mtu awe na mawasiliano ya simu na
mwezake jambo ambalo litasaidia kupeana taarifa pindi uhalifu
unapotokea.
Katika
kuhamasisha kufufua vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi Mkuu huyo wa Polisi
Wilaya alianzisha harambee ya kuchangisha fedha kwa kila mkazi aliyehudhuria
mkutano huo hali ambayo ilisaidia kupatikana kwa fedha taslimu Tsh 125,000 papo
hapo huku yeye mwenyewe akiwa wa kwanza kutoa mchango
wake.
Aliongeza kwa kuwaambia
wananchi hao katika kuimarisha vikundi hivyo, wanatakiwa wafanye jitihada za
kupata sare zitakazowatambulisha, filimbi na bunduki mbili ambazo zitatumiwa na
askari wa doria ambao watakuwa wamepata mafunzo ya Mgambo. Alisema katika suala
usajili wa bunduki hizo yeye atakuwa mstari wa mbele kupeleka maombi yao kwa
viongozi wa juu ili waweze kupitisha na hatimaye ziweze kutumika kwenye shughuli
ya ulinzi katika eneo lao.
Kwa
upande mwingine aliwataka mabalozi wa eneo hilo kutafuta askari watakaokuwa
waaminifu ili waweze kufanya kazi zao kwa uadilifu. Mbali na hilo aliwataka
viongozi hao kubuni miradi ya uzalishaji mali ambayo itakuwa moja ya chanzo cha
mapato ya malipo kwa askari hao badala ya kutegemea michango ya wananchi
pekee.
Muroto
alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa eneo hilo kushirikiana na Jeshi la polisi
katika kutoa taarifa zinazohusu uhalifu, ambapo alitoa namba za simu za viongozi
wa Jeshi la Polisi mkoani hapa ili ziweze kusaidia kushirikiana kimawasiliano
katika suala hilo. Pia aliahidi kurudi tena katika eneo hilo pamoja na timu yake
kutoa elimu kwa askari watakaoteuliwa kabla hawajaanza kazi rasmi ili waweze
kujua misingi na mbinu mbalimbali za utendaji wa kazi hiyo na hilo ni moja ya
jukumu la Jeshi la Polisi kwa vikundi hivyo.
Awali Mwenyekiti wa
Mtaa wa Kitalu “D” Bw. John kihwele akifungua mkutano huo, alisema kwamba
vikundi vya ulinzi shirikishi vilikuwepo lakini kilichochangia vikundi hivyo
kuyeyuka ni ugumu wa wakazi hao kuchangia vikundi hivyo.
Alisema
pamoja na uwepo wa walinzi karibu kila nyumba lakini uwepo wa vikundi vya ulinzi
shirikishi ni wa umuhimu sana hasa katika kufanya doria za barabara hali ambayo
itasaidia kuimarika kwa ulinzi.
Tuesday, November 13, 2012
Saturday, November 3, 2012
UBUNGO PLAZA HAPOTOSHI!
LEO NDIO LEO REDDS MISS TANZANIA 2012 NDANI YA UBUNGO PLAZA
CAREN ELIAS mshiriki 23
anatokea Mbeya anawakilisha Nyanda za Juu Kusini
BRIGITTE ALFRED ni
Mshiriki namba 26 akitokea Kitongoji cha Sinza na anawakilisha Kanda ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Anaitwa VIRGINIA MOKIRI ni
mshiriki namba 1. Akitokea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na akiwakilisha Elimu ya
Juu.
Anakwenda kwa jina
la EUGENE FABIAN
Mbio za kulisaka taji la Miss Tanzania amezianzia Mkoani Mara na baade
kutwaa taji la Kanda ya Ziwa na anavalia namba 21 kambi ya
taifa.
BABYLOVE KALALA ni Mshiriki
na 9 akitokea mkoa wa Kagera, akiwakilisha Kanda ya Ziwa.
ANANDE RAPHAEL ni mshiriki
namba 11 akitokea Mkoa wa Kilimanjaro akiwakilisha Kanda ya
Kaskazini.
CATHERINE MASUMBIGANA ni mshiriki na 15 akitokea Kitongoji cha Chang'ombe anawakilisha kanda uya Temeke jijini Dar es Salaam.
DIANA HUSSEIN amepata namba
ya ushirtiki 20, akitokea kitongoji cha Dar Indian Ocean, akiiwakilisha Kanda ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
FINA REVOCATUS anavaa namba
12 akitoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, akiwakilisha Kanda ya Vyuo Vya Elimu
ya Juu.
BELINDA MBOGO ni mshiriki
na 29 akitoka mkoa wa Dodoma akiwaklilisha Kanda ya Kati
EDDA SYLVESTER amepata
namba 22, akitoka Kigamboni na anaiwakilisha Kanda ya Temeke jijini Dar es
Salaam.
ELIZABETH DIAMOND anavalia
namba 2 akitokea mkoa wa singida, akiwakilisha kanda ya Kati.
FATMA RAMADHANI nambari
yake 25 akitoka chuo cha Uandishi wa habari Arusha ASJ, anawakilisha Kanda ya
Elimu ya Juu.
FLAVIAN MAEDA anavalia
namba 10 akitokea kitongoji cha Kurasini mwakilishi wa kanda ya Temeke jijini
Dar es Salaam.
Kutoka Kahama- Shinyanga ni
HAPPINESS RWEYEMAMU ananamba 8 anawakilisha Kanda ya Ziwa.
Huyu ni HAPPYNESS DANIEL
namba yake ya ushiriki ni 19 anatokea jiji la Mwanza akiwakilisha Kanda ya
Ziwa.
IRINE VEDA anatokea Lindi
na kupata namba 16 akiuwakilisha Kanda ya Mashariki
JESCA HAULE ni mshiriki
namba 14, akitoka kitongoji cha Chang'ombe anawakilisha Kanda ya Temeke jijini
Dar es Salaam.
Anatoka Mji kasoro
Bahari-Morogoro ni JOYCE BALUHI akiwa ni mshiriki 13 anawakilisha Kanda ya
Mashariki.
KUDRA LUPATOni
mshiriki 24 akitokea kitongoji cha Dar Indian Ocean, akiiwakilisha Kanda ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Huyu ni LIGHTNESS MICHAEL
anavalia 5, akitokea Dodoma akiwakilisha Kanda ya Kati.
Kutoka mkoa wa Manyara ni
LUCY STEPHANO mshiriki namba 4 akiwakilisha Kanda ya Kaskazini.
MAGDALENA ROY mshiriki
namba 6, kutoka Kitongoji cha Dar City Centre akiwakilisha Kanda ya
Ilala.
Anaitwa Mary Chizi akitokea
kitongoji cha Ukonga, anavalia namba 17, akiwakilisha Kanda ya Ilala jijini Dar
es Salaam.
Yeye ni MAGDALENA ROY
mshiriki nambari 18, kutyoka mkoa wa Iringa akiwakilisha Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini.
Jinalake ni NOELA MICHAEL
yupo na namba 27, anashikilia taji la kitongoji cha Tabata na ni mwakilishi
tegemeo wa Kanda ya Ilala.
Rose Lucas ana namba 28
akitokea Mkoa wa Pwani akiwakilisha Kanda ya Mashariki
VENCY EDWARD ni mshiriki
nambari 7, akitoka Mkoa wa Rukwa akiwakilisha Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini
WARID FRANK huyu ni
mshiriki namba 30 akitokea Arusha ana kuiwakilisha Kanda ya
Kaskazini.
Anaitwa ZUWENA NASIB akiwa
ni mwakilishi pekee wa chuo Kikuu Huria OUT
Wednesday, October 31, 2012
NYOTA 23 WAWANIA TUZO YA FIFA
ORODHA YA NYOTA 23 WANAOWANIA TUZO YA FIFA Ballon d'Or.... AFRIKA NZIMA WAMO DIDIER DROGBA NA YAYA TOURE TU... REAL MADRID YATOA NYOTA SITA, BARCELONA YATOA WACHEZAJI WATANO, MANCHESTER CITY WATATU....!
ZURICH,
Usiwsi
STRAIKA wa timu ya taifa ya Argentina na
klabu ya Barcelona, Lionel Messi yuko mbioni kuandika rekodi ya kuwa mtu wa
kwanza kushinda tuzo ya Mwansoka Bora wa Mwaka wa Dunia kwa mara ya nne
mfululizo baada ya kujumuishwa katika orodha iliyotolewa leo na Shirikisho la
Soka la Kimataifa (FIFA) kuwania tuzo hiyo ya
Straika huyo mwenye miaka 25, aliyeongeza
idadi ya mgoli yake tangu aanze kucheza akiwa na klabu na timu ya taifa hadi
kufikia 301 Jumamosi, ni miongoni mwa nyota 23 waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo,
wengine wakiwa ni hasimu wake, straika wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa
ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ambaye alishika nafasi ya pili katika tuzo
zilizotolewa mwaka jana na Messi kuibuka kidedea.
Andres Iniesta wa Barcelona, aliyetajwa kuwa
mchezaji bora wa fainali za Euro 2012 baada ya kuisaidia Hispania kutwaa ubingwa
pia amejumuishwa katika orodha hiyo kama ilivyo kwa Radamel Falcao, ambaye
amekuwa akionyesha kiwango cha juu cha upachikaji mabao akiwa na timu yake ya
taifa ya Colombia na klabu ya Atletico Madrid, akiisaidia nchi yake kutwaa
ubingwa wa Ligi ya Europa msimu uliopita.
Kocha wa Barca, Tito Vilanova amemwagia sifa
Messi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo.
"Sidhani kama tutapata nafasi ya kuona tena
mchezaji kama yeye. Sio tu kwa sababu ya mabao anayofunga lakini pia kwa uwezo
wake wa kusoma mchezo," alisema kabla ya kumsiofia pia Iniesta.
"Yeye (Iniesta) ni mfano kwa wachezaji
wanaolelewa Masia (shule ya soka ya vijana wa Barcelona) na kufikia kiwango cha
juu. Ni mchezaji mwingine miongoni mwa wenye viwango vya juu na ambao Barca
itapata wakati mgumu wa kuwaibua tena."
Makocha 10 pia wametajwa kuwania Tuzo ya
Kocha Bora wa Mwaka wa Dunia, akiwamo Vicente del Bosque, aliyeiongoza Hispania
kutwaa ubingwa wa fainali za Euro 2012 zilizofanyika Julai nchini Ukraine na
Poland.
Roberto Di Matteo, aliyetwaa nafasi ya
kuiongoza Chelsea miezi miwili kabla ya kutwaa taji la Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya mwezi Mei, pia amejumuishwa katika orodha hiyo ambayo hata hivyo
haikumjumuisha Mfaransa Herve Renard aliyeiongoza Zambia kutwaa ubingwa bila
kutarajiwa katika fainali za Kombe Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi
Februari.
Orodha hiyo fupi itachujwa zaidi na kubaki
watu watatu kufikia mwishoni mwa Novemba huku mshindi akitarajiwa kutangazwa
duniani kote kupitia matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya sherehe za
kukabidhi tuzo zitakazofanyika mjini Zurich, Uswisi Januari 7 mwakani.
Wachezaji (kwa kuzingatia mpangilio wa herufi
za majina yao):
1. Sergio Aguero (Argentina)
2. Xabi Alonso (Hispania)
3. Mario Balotelli (Italia)
4. Karim Benzema (Ufaransa)
5. Gianluigi Buffon (Italia)
6. Sergio Busquets (Hispania)
7. Iker Casillas (Hispania)
8. Cristiano Ronaldo (Ureno)
9. Didier Drogba (Ivory Coast)
10. Radamel Falcao (Colombia)
11. Zlatan Ibrahimovic (Sweden)
12. Andres Iniesta (Hispania)
13. Lionel Messi (Argentina)
14. Manuel Neuer (Ujerumani)
15. Neymar (Brazil)
16. Mesut Ozil (Ujerumani)
17. Gerard Pique (Hispania)
18. Andrea Pirlo (Italia)
19. Sergio Ramos (Hispania)
20. Wayne Rooney (England)
21. Yaya Toure (Ivory Coast)
22. Robin van Persie (Uholanzi)
23. Xavi (Hispania).
Makocha (kwa kuzingatia herufi za kwanza za
majina yao pili):
1. Vicente del Bosque (Hispania/taifa
Hispania)
2. Roberto Di Matteo
(Italia/Chelsea)
3. Alex Ferguson (Scotland/Manchester
United)
4. Pep Guardiola (Hispania/kocha wa zamani
Barcelona)
5. Jupp Heynckes (Ujerumani/Bayern
Munich)
6. Jurgen Klopp (Ujerumani/Borussia
Dortmund)
7. Joachim Low (Ujerumani/taifa
Ujerumani)
8. Roberto Mancini (Italia/Manchester
City)
9. Jose Mourinho (Ureno/Real
Madrid)
10. Cesare Prandelli (Italia/taifa
Italia)
AZAM YAMTIMU KOCHA WAO
AZAM FC YAMTIMUA KOCHA WAKE BORIS BUNJAK
Kocha wa
Azam FC mserbia Boris Bunjak ametimuliwa rasmi kuifundisha
timu hiyo.
Taarifa rasmi nilizozipata kutoka ndani ya
klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya VPL zinasema kwamba kocha huyo aliyesaini
mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Azam mwezi nane mwaka huu ametimuliwa na
sasa viongozi wa klabu hiyo wapo katika harakati za kutaka kumrudisha kocha wao
wa zamani Muingereza Stewart Hall.
Hatua hii imekuja siku mbili baada ya Azam
FC kufungwa 3-1 na Simba katika mechi ya ligi kuu.

NYOTA 23 WAWANIA TUZO YA FIFA Ballon d'Or...
ORODHA YA NYOTA 23 WANAOWANIA TUZO YA FIFA Ballon d'Or.... AFRIKA NZIMA WAMO DIDIER DROGBA NA YAYA TOURE TU... REAL MADRID YATOA NYOTA SITA, BARCELONA YATOA WACHEZAJI WATANO, MANCHESTER CITY WATATU....!
ZURICH,
Usiwsi
STRAIKA wa timu ya taifa ya Argentina na
klabu ya Barcelona, Lionel Messi yuko mbioni kuandika rekodi ya kuwa mtu wa
kwanza kushinda tuzo ya Mwansoka Bora wa Mwaka wa Dunia kwa mara ya nne
mfululizo baada ya kujumuishwa katika orodha iliyotolewa leo na Shirikisho la
Soka la Kimataifa (FIFA) kuwania tuzo hiyo ya
Straika huyo mwenye miaka 25, aliyeongeza
idadi ya mgoli yake tangu aanze kucheza akiwa na klabu na timu ya taifa hadi
kufikia 301 Jumamosi, ni miongoni mwa nyota 23 waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo,
wengine wakiwa ni hasimu wake, straika wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa
ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ambaye alishika nafasi ya pili katika tuzo
zilizotolewa mwaka jana na Messi kuibuka kidedea.
Andres Iniesta wa Barcelona, aliyetajwa kuwa
mchezaji bora wa fainali za Euro 2012 baada ya kuisaidia Hispania kutwaa ubingwa
pia amejumuishwa katika orodha hiyo kama ilivyo kwa Radamel Falcao, ambaye
amekuwa akionyesha kiwango cha juu cha upachikaji mabao akiwa na timu yake ya
taifa ya Colombia na klabu ya Atletico Madrid, akiisaidia nchi yake kutwaa
ubingwa wa Ligi ya Europa msimu uliopita.
Kocha wa Barca, Tito Vilanova amemwagia sifa
Messi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo.
"Sidhani kama tutapata nafasi ya kuona tena
mchezaji kama yeye. Sio tu kwa sababu ya mabao anayofunga lakini pia kwa uwezo
wake wa kusoma mchezo," alisema kabla ya kumsiofia pia Iniesta.
"Yeye (Iniesta) ni mfano kwa wachezaji
wanaolelewa Masia (shule ya soka ya vijana wa Barcelona) na kufikia kiwango cha
juu. Ni mchezaji mwingine miongoni mwa wenye viwango vya juu na ambao Barca
itapata wakati mgumu wa kuwaibua tena."
Makocha 10 pia wametajwa kuwania Tuzo ya
Kocha Bora wa Mwaka wa Dunia, akiwamo Vicente del Bosque, aliyeiongoza Hispania
kutwaa ubingwa wa fainali za Euro 2012 zilizofanyika Julai nchini Ukraine na
Poland.
Roberto Di Matteo, aliyetwaa nafasi ya
kuiongoza Chelsea miezi miwili kabla ya kutwaa taji la Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya mwezi Mei, pia amejumuishwa katika orodha hiyo ambayo hata hivyo
haikumjumuisha Mfaransa Herve Renard aliyeiongoza Zambia kutwaa ubingwa bila
kutarajiwa katika fainali za Kombe Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi
Februari.
Orodha hiyo fupi itachujwa zaidi na kubaki
watu watatu kufikia mwishoni mwa Novemba huku mshindi akitarajiwa kutangazwa
duniani kote kupitia matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya sherehe za
kukabidhi tuzo zitakazofanyika mjini Zurich, Uswisi Januari 7 mwakani.
Wachezaji (kwa kuzingatia mpangilio wa herufi
za majina yao):
1. Sergio Aguero (Argentina)
2. Xabi Alonso (Hispania)
3. Mario Balotelli (Italia)
4. Karim Benzema (Ufaransa)
5. Gianluigi Buffon (Italia)
6. Sergio Busquets (Hispania)
7. Iker Casillas (Hispania)
8. Cristiano Ronaldo (Ureno)
9. Didier Drogba (Ivory Coast)
10. Radamel Falcao (Colombia)
11. Zlatan Ibrahimovic (Sweden)
12. Andres Iniesta (Hispania)
13. Lionel Messi (Argentina)
14. Manuel Neuer (Ujerumani)
15. Neymar (Brazil)
16. Mesut Ozil (Ujerumani)
17. Gerard Pique (Hispania)
18. Andrea Pirlo (Italia)
19. Sergio Ramos (Hispania)
20. Wayne Rooney (England)
21. Yaya Toure (Ivory Coast)
22. Robin van Persie (Uholanzi)
23. Xavi (Hispania).
Makocha (kwa kuzingatia herufi za kwanza za
majina yao pili):
1. Vicente del Bosque (Hispania/taifa
Hispania)
2. Roberto Di Matteo
(Italia/Chelsea)
3. Alex Ferguson (Scotland/Manchester
United)
4. Pep Guardiola (Hispania/kocha wa zamani
Barcelona)
5. Jupp Heynckes (Ujerumani/Bayern
Munich)
6. Jurgen Klopp (Ujerumani/Borussia
Dortmund)
7. Joachim Low (Ujerumani/taifa
Ujerumani)
8. Roberto Mancini (Italia/Manchester
City)
9. Jose Mourinho (Ureno/Real
Madrid)
10. Cesare Prandelli (Italia/taifa
Italia)
AZAM YARUDIA MATAPISHI
AZAM YAAMUA KUMRUDISHA STEWART HALL BAADA YA JANA KUMTIMUA BUNJAK
azam
baada yakumtmua kocha wao mserbia Boris Bunjak
imeamua kumrudisha kocha wake wa zamani mwingereza Stewart Hall aneifundisha Sofapaka ya Kenya
kwasasa. hii imedhibitishwa kwakuandika
katika page yao ya facebook kakuandika hivi
Tangazo
Azam FC imeamua
kuvunja mkataba na kocha Boris Bunjak na kumrejesha kazini Stewart Hall, hii
imetokana na Maombi na Maoni ya mashabiki pamoja na wataalam wa mambo ya ufundi
mbalimbali ambao walitoa maoni kuwa ni vema tukamrejesha kocha Stewart
Hall.
Azam
imeamua kumtimua mserbia huyo baada ya kuonyesha kiwango duni
Kocha alietimuliwa Boris Bunjak |
CHEKI VIJANA WA SIMBA WAKIWA MAZOEZINI HUKO JAMHURI HAPO JANA
EMMANUEL OKWE
KUSHOTO AKIPIMANA UBAVU NA FELIX ZUNZU WAKATI WA MAZOEZI YA KLABU YA SIMBA KWA
AJILI YA MCHEZO BAINA YA TIMU HIYO NA POLISI MORO SC KATIKA LIGI KUU YA VODACOM
TANZANIA BARA JIONI KATIKA UWANJA WA JAMHURI
MOROGORO.
DANIEL AKUFF (KATIKATI) AKIWA AMENYANYUA
DALUGA WAKATI AKIWANIA MPIRA DHIDI YA AMRI KIHEMBA KULIA HUKU HARUNA SHAMTE
AKIUPIGIA MAHESABU MPIRA HUO.
UHURU SELEMAN (16) AKITAFUTA NAMNA YA
KUWATOKA WACHEZAJI WENZAKE MWINYI KAZIMOTO.
WACHEZAJI WAKIOMBA DUA MARA BAADA YA
KUMALIZIKA KWA MAZOEZI.
MASHABIKI WA KLABU YA SIMBA WAKINGALIA MAZOEZI
YA KLABU HIYO.
KIKOSI cha simba leo kimefanya mazoezi katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
nakuwa kivutio zaidi kwa wakazi wa Morogoro ambao walijitokeza kwa wingi
uwanjani hapo.
Simba ipo mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo
dhidi ya Polisi Moro na ipo full kwa mchezo huo utakaopigwa
kesho
Subscribe to:
Posts (Atom)